Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thomas Tuchel: Hatupaswi Kuendelea Kukosea

Tuchel T Meneja wa Chelsea, Thomas Tuchel

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu Thomas Tuchel amekiri kwamba Chelsea hawapaswi kuendelea kufanya makosa baada ya kichapo cha 3-2 kutoka kwa West Ham United.

Licha ya The Blues kuongoza mara mbili, makosa ya kipa Edouard Mendy yaliwazawadia West Ham penalti, huku mlinda mlango wa Senegal akishindwa kuzuia mpira wa krosi wa Arthur Masuaku kuingia ndani ya lango.

Licha ya juhudi za kuusaka ushindi, na makosa ya wazi kutoka kwa Mendy, Chelsea ilifanya makosa mengine kadhaa kama timu, jambo ambalo Tuchel alilitaja kwa haraka baada ya kumalizika kwa mechi.

“Sidhani kama tulicheza vibaya, mechi ilikuwa sawa, tunaweza kushinda kwa uchezaji huu.”

“Ni ngumu kucheza hapa, tulifanya makosa mengi ya binafsi. Tayari tulifanya dhidi ya Manchester United na Watford na tukaadhibiwa, ikiwa unataka matokeo katika kiwango hiki lazima upunguze makosa.”

Akizungumzia penalti ya kipindi cha kwanza, Mjerumani huyo aliongeza: “Kila mtu anahusika, pasi si uamuzi bora, mwelekeo si bora, tunaweza kulinda lakini maamuzi pia hayakuwa bora kwa Edu katika hili.”

Chelsea itashuka hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Premier League ikiwa Manchester City na Liverpool wataweza kuwachapa Watford na Wolverhampton Wanderers.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live