Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thomas Partey aivimbia Manchester City

Thomas Partey Miss.jpeg Thomas Partey

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: Dar24

Kiungo kutoka nchini Ghana na Klabu ya Arsenal Thomas Teye Partey amesema wapo tayari kwenda katika Uwanja wa Etihad kupambana na kupata matokeo yatakayowaweka katika Ramani ya Ubingwa msimu huu 2022/23.

Arsenal itakua mgeni wa Man City keshokutwa Jumatano (April 26) ikiwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha inashinda ili kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Partey amesema anaamini kikosi cha Arsenal kipo katika mazingira mazuri ya kwenda kupambana ugenini na kupata matokeo, licha ya kukabiliwa na matokeo ya sare kwenye michezo mitatu iliyopita.

Amesema wanatambua umuhimu wa mchezo huo wa Jumatano, kwani ndio umeshikilia hatma ya kuendelea kukaa kileleni sambamba na kuendelea kuwa katika vita ya Ubingwa.

“Kila kitu kipo kipo kwenye uwezo wetu, tunapaswa kwenda Eithad na kushinda mchezo huo, inawezekana kushinda ikiwa tutaenda na mbinu zetu za kucheza tulizoanza nazo toka mwanzo na tukaenda kucheza mpira mzuri tutashinda.

“Watu hatupaswi kukataa tamaa juu ya EPL mimi nina uhakika tutashinda dhidi ya City na kuchukua ubingwa wa ligi kuu England”. Amesema Partey

Hadi sasa Arsenal inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa na alama 75, ikifuatiwa na Man City yenye alama 70 huku ikiwa na michezo miwili mkononi.

Arsenal iliingia katika sintofahamu ya kuendelea kuwa kileleni baada ya kuambulia sare ya 3-3 dhidi ya Southampton Ijumaa (April 21) katika Uwanja wa Emirates jijini London.

Kabla ya hapo Arsenal iliambulia sare ya 2-2 dhidi ya West Ham Utd na Liverpool zilizokuwa katika viwanja vya nyumbani.

Chanzo: Dar24