Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thierry Henry awachana PSG juu ya Mbappe

Thierry Mbappe Thierry Henry akiwa na Mbappe

Mon, 13 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa Arsenal na Ufaransa, Thierry Henry amewatolea uvivu PSG juu ya hali ya mkataba wa nyota wao Kylian Mbappe.

Mpappe anaelekea kumaliza mkataba wake na PSG, na hii inaweza kuwa fursa ya Real Madrid kumsajili staa huyu baada ya kumfukuzia kwa mda mrefu na jitihada zao kugonga mwamba.

Ikiwa hali itakuwa hivi, na Mbappe atakuwa hajasaini makubaliano mapya na PSG, Real Madrid wanaweza kukubaliana masharti ya awali na kinda huyu wa Ufaransa mwezi Januari.

Mpappe amekuwa akiwa shabiki wa Real Madrid, na ni ndoto aliyokuwa nayo siku moja kuwepo Madrid kuichezea timu yake pendwa, hii inaonesha kuwa Mbappe hawezi kuwa mzito kumwaga wino, fursa inapotokea.

Lakini kwa mujibu wa Thierry Henry, suala hili PSG wamekwama, walihitaji kulitambua na kulifanyia kazi mapema zaidi. Amenukuliwa akisema;

“Hali hii ilipaswa kutatuliwa miaka miwili iliyopita. Misimu miwili iliyopita walipaswa kukaa chini na Mbappe kumwambia: ‘Hii itakuwa timu yako, tutaijenga timu hii ni wewe, utakuwa kiongozi.’” Thierry Henry

“Sasa, ana hatima yake ipo mikononi mwake mwenyewe. Angeweza kusaini anapotaka, lakini hili lilipaswa kuwekwa sawa muda mrefu uliopita.” Thierry Henry

Chanzo: www.tanzaniaweb.live