Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Thibaut Courtois kipa bora Duniani’ – Ancelotti

Thibaut Courtois 1536x864 Thibaut Courtois

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelotti anaamini Thibaut Courtois ndiye mlinda mlango bora katika ulimwengu wa soka kwa sasa.

Mazungumzo kuhusu ‘nani bora zaidi’ yameshika kasi wiki hii wakati kukiwa na shughuli ya utoaji tuzo za Ballon d’Or.

Kama sehemu ya sherehe hiyo, Yashin Trophy ilitolewa, na tuzo hiyo inatolewa kwa kipa bora kwa msimu uliopita.

Kama vile Ballon d’Or, hii pia hupigiwa kura na waandishi wa habari, na ilishangaza wengi kwamba mlinda mlango wa Real Madrid Courtois alimaliza akiwa nafasi ya nane, nyuma ya Kasper Schmeichel na Emiliano Martinez.

Wakati huo huo, kipa wa PSG Gianluigi Donnarumma ndiye aliyeshinda tuzo kama mlinda mlango bora.

Lakini bila kujali tuzo hizo, bosi wa Real Madrid, Ancelotti anaamini Courtois ndiye kipa bora kwa sasa kwenye ulimengu wa soka.

Ancelotti alisema: “Tumekuwa na bahati kuwa na walinda mlango wazuri. Casillas, Diego Lopez, Buffon, Cech, Neuer. Tribu ni miongoni mwa bora bila shaka na yeye ndiye bora kwa sasa.”

Courtois amekuwa na Real Madrid tangu mwaka 2018 akitokea Chelsea, na amekuwa akipokea maoni mazuri tangu wakati huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live