Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

The Gunners waishusha Man United Top Four

Top Four Man United Arsenal waichapa Leicester goli 2-0

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Arsenal imeendeleza vichapo kwenye Ligi Kuu England na kurejea kwenye nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi hiyo baada ya kuichapa Leicester City goli 2-0.

Ushindi wa The Gunners unakuwa wa tano mfululizo kwenye mechi za Ligi Kuu ambapo wanafikisha alama 51 katika nafasi ya nne juu ya mashetani wekundu Manchester United ambao walishinda jana Jumamosi bao 3-2 dhidi ya Tottenham.

Thomas Partey alitangulia kuifungia Arsenal akimalizia mpira wa kona wa Gabriel Martinelli kabla ya kupata goli la pili kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati uliopigwa na nahodha Alexandre Lacazette.

Kwa matokeo hayo, Leicester City wanabakia nafasi ya 12 kwenye msimamo wa EPL, inakuwa mara ya kwanza kupoteza mechi mbili nyumbani na ugenini tangia msimu wa 2015/16.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live