Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thank you zinaendelea Simba SC

Ahmed Ally 23 Thank you zinaendelea Simba SC

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulikuwa unafikiri zoezi la kuwaaga wachezaji ambao hawana mpango wa kuendelea nao Simba SC limefikia tamati taarifa ikufikie kwamba bado, zoezi linaendelea wiki hii.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema, mpaka sasa wamechatangaza kuachana na nyota sita na wiki hii wanakwenda kukamilisha zoezi hilo kwa kuachana na wengine.

"Tumeshaachana na nyota wetu sita mpaka sasa ambao ni Okrah, Okwa, Akpan, Mkude Erasto na Beno Kakolanya. Wiki hii tunaendelea na zoezi kwa sababu wapo wachezaji ambao bado wana mikataba hivyo huwezi kutangaza tu unaachana nao kirahisi.

"Tunafanya mazungumzo, wapo ambao tutazungumza nao tuwatoe kwa mkopo hivyo lazima tumalizane nao wao pamoja na timu zinazowahitaji," alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live