Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thank you Jobe, welcome Makusu

Jobe Makusu Jobe na Makusu.

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi wanatajwa wako katika mipango ya kumsajili straika, Jean-Marc Makusu Mundele, kutoka DC Motemba Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), imefahamika.

Hii ni mara ya pili kwa Simba kufanya mchakato wa kumsajili straika huyo ambaye ni raia wa DRC, baada ya kushindwa kukamilisha dili hilo msimu uliopita.

Straika huyo wa zamani wa Klabu za AS Vita, St. Eloi Lupopo na Orlando Pirates ya Afrika Kusini, kwa sasa anaichezea Hajer FC ya Saudi Arabia.

Habari kutoka ndani ya Simba zinasema straika huyo anaweza kutua kuchukua nafasi ya mshambuliaji, Pa Omari Jobe, ambaye huenda akaachwa mara baada ya msimu huu kumalizika.

Naye Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema wameamua kuipeleka Arusha mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC kutokana na sababu za 'kimkakati' licha ya awali kuomba ichezwe kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

"Kuna sababu mbili au tatu kubwa kubwa zilizotufanya tuipeleke mechi Arusha, kwanza kabisa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid umekuwa na bahati kubwa sana kwetu, kwani mara ya mwisho katika mechi ya Ligi Kuu kwenye uwanja huo tuliifunga Coastal Union mabao 7-0, na kwa vile tuna uhitaji wa mabao mengi, tumeamua kuileta huku.

Pili ni wanachama na mashabiki wa Arusha hawajaiona timu yao ikicheza 'laivu' kwa muda mrefu, mara ya mwisho ilikuwa ni Novemba, 2020 pale tulipocheza dhidi ya Coastal Union, sasa ni miaka minne imepita, mashabiki wa Simba Arusha wanaishia kuiona kwenye televisheni, tumeona wacha tuwapelekee na wao waende wakaione, na hiyo ni sababu ya kwanza iliyotufanya tuilete huku," alisema Ahmed.

Katika ushindi wa 7-0, mechi iliyochezwa Novemba 21, 2020 straika, John Bocco alifunga hat-trick, mabao mawili yakifungwa na Clatous Chama huku Hassan Dilunga na Benard Morrison wakifunga bao moja kila mmoja.

"Nyote mnafahamu tupo katika vita kubwa ya kuwania tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, nyote mnafahamu zilizosalia ni mechi za maamuzi na ngumu, hivyo lazima uzipeleke kwa watu wagumu ambao wanaweza kufanya mambo ili Simba kupata ushindi na watu wa aina hii wanapatikana Arusha," alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live