Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thamani ya milionl 600 kaitengeneza kwa jasho lake, aheshimiwe - Dauda

Kibu D KIBU DENGA.jpeg Kibu Denis.

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kibu kaitengeneza mwenyewe thamani yake hadi hapo ilipo leo, unaposema hana thamani hiyo anayoitaja yeyeni kumkosea heshima.

Kibu anaamini thamani yake kwa sasa ni zaidi ya Tsh. 600 milioni, kama klabu itaona hana thamani hiyo itamwacha aondoke.

Kibu Denis ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na juzi tu ametoka kucheza AFCON, amecheza mechi za African Football League na CAF Champions League.

Kuna uwezekano mkubwa akawa na ofa kutoka klabu za mataifa mengine [Misri, Morocco, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu nk], kwa sababu kacheza mashindano ya kimataifa vizuri na kaonekana.

Mfano Pyramids au Wydad ikimtaka Kibu, hawawezi kutoa zaidi ya Tsh 600 milioni? Kwa hiyo inategemea Kibu ana ofa kutoka timu za mataifa gani lakini maraifa kama Misri, Morocco, Qatar, Saudi Arabia kumpa mchezaji kiasi kikubwa cha pesa wala sio jambo la kushangaza sana.

Platform ambayo Kibu ameipata akiwa Simba na Taifa Stars ni kubwa, kwa hiyo inawezekana ana ofa nyingi ndani na nje ya nchi lakini ukiwaza Kibu ana ofa ya Simba, Yanga au Azam tu ndio hapo utaona Tsh. 600 milioni ni nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live