Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thamani mpya za mastaa waliosajiliwa dirisha lililopita

James Maddison: Tottenham James Maddison

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wachezaji wenye faida na thamani kubwa waliosajiliwa katika Ligi Kuu ya England katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi lililopita imefichuliwa kwa mujibu wa Gazeti la Sun.

Mastaa hawa wapya wanaposajiliwa wanaleta hofu kwani kuna uwezekano wakashindwa kupiga hatua kubwa kwenye timu, bila kujali jina, umri na hiyo tumeshuhudia kwa baadhi ya mastaa, waliosajiliwa katika madirisha ya usajili la kiangazi yaliyopita akiwemo Antony anayekipiga Manchester United, Darwin Nunez (Liverpool), Kai Havertz ambaye sasa anaichezea Arsenal na wengine wengi.

Lakini, wataalamu wa data katika Punter’s Pub wamefichua ni usajili gani bora wa kiangazi ambao ulifanyika mwaka huu ambao umeleta faida zaidi kwa timu za Ligi Kuu England baada ya michezo 11 ya kwanza ya msimu. Ikishirikisha nyota wa zamani wa Chelsea na Manchester United, orodha hiyo ina majina kadhaa yanayofahamika.

Akianza akiwa na nafasi ya 10 kwenye orodha, chipukizi wa zamani wa Man United, Anthony Elanga ameboresha thamani yake ya uhamisho tangu alipohamia Nottingham Forest kutokana na ubora wake.

Elanga 21, amefunga bao moja na kutengeneza (asisti) mabao matatu kwa upande wa Kocha Steve Cooper tangu alipohamia Forest Ground kwa Pauni 15.2 milioni.

Uchezaji wake tumeona umeongezeka dogo la asilimia tatu na kufikisha thamani yake sokoni hadi kufikia Pauni 15.6 milioni.

Nyota wa Fulham, Alex Iwobi ndiye anayefuata akiwa na ongezeko la asilimia tisa tangu kukamilisha uhamisho wake wa Pauni 2.3 milioni kutoka Everton na kufikisha thamani ya nyota huyo wa zamani wa Arsenal hadi kufikia Pauni 24.3 milioni.

Nyota wa Bournemouth, Justin Kluivert anafuatia baada ya thamani yake kupanda kwa asilimia 25 hadi kufikia Pauni 12.1 milioni - huku Bournemouth ikilipa Pauni 9.7 milioni ilipomsajili dirisha la usajili la kiangazi lililopita na hiyo ni kutokana ubora wake msimu huu.

Mchezaji mpya wa Burnley, Michael Obafemi anafuata kwenye orodha hii ya wachezaji hatari waliosajilia amabo tayari wameleta matunda kwa timu zao.

Mchezaji huyo 23, pia, ameshuhudia ongezeko la thamani yake kupanda kufikia Pauni 25 asilimia, akiwa chini ya kikosi cha Vincent Kompany cha chenye thamani ya Pauni 3.5 milioni ambapo pia alisajiliwa kwa Pauni 4.3 milioni alipotua dirisha la usajili la kiangazi.

Mchezaji mwingine hatari wa Chelsea, Christopher Nkunku pia ameshuhudia ongezeko la thamani ya uhamisho wake licha ya kuwa bado hajacheza mechi hata moja kutokana na majeraha na hivi karibuni atadhihirisha ubora wake wa kupachika mabao chini ya Kocha Mauricio Pochettino.

Nyota huyo wa zamani wa RB Leipzig thamani yake imepanda kwa asilimia 33 na kumpa thamani sokoni hadi kufikia Pauni 69.4 milioni - zaidi ya Pauni 52 milioni walizotoa Chelsea.

Jacob Brown wa Luton ndiye anayefuata, baada ya kuletwa kutoka Stoke City kwa Pauni 2.5 milioni. Lakini Brown (25) kwa sasa ana thamani ya Pauni 3.4 milioni kufuatia ongezeko la asilimia 38 la thamani yake.

Nyota wa Tottenham, James Maddison ndiye anayefuata kwenye orodha hiyo baada ya kuanza maisha mazuri Kaskazini mwa London.

Maddison alihamia Spurs kutoka Leicester City kwa Pauni 40.1 milioni, lakini sasa ana thamani ya Pauni milioni 60.7 milioni - ongezeko la asilimia 51 katika thamani yake baada ya kufunga mabao matatu na na asisti tano za mabao katika mechi 11 za mwanzo za Ligi Kuu England.

Mchezaji mwenzake wa Spurs, Dejan Kulusevski ndiye anayefuata baada ya kusaini mkataba wa kudumu na klabu hiyo kwa Pauni 26 milioni 26 kipindi cha usajili wa kiangazi na amekuwa na mchango mkubwa akiwa na timu hiyo inayonolewa na kocha mpya Ange Postecoglou ambaye wikeindi iliyopita alipokea kichapo cha kwanza cha msimu dhidi ya Chelsea kwani ilijikuta ikichezea kichapo cha mabao 4-1.

Winga huyo amepanda thamani yake na kufikisha Pauni 67 milioni - awali thamani yake ilikuwa Pauni 43.4 milioni. Nyota mwingine wa Burnley, Luca Koleosho, ambaye alisajiliwa na na timu hiyo kwa Pauni 2.6 milioni na sasa thamani yake imependa hadi 5.2 milioni baada ya kupanda kwa asilimia 100.

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Callum Hudson-Odoi. Nyota huyo alinunuliwa na Nottingham Forest kwa Pauni 3 milioni tu baada ya kuvumilia Stamford Bridge kabla ya kutolea kwa mkopo.

Usajili wake umetoa faida kubwa kwa Nottingham - ikiwa ni pamoja na bao lake la kushangaza dhidi ya Burnley. Hii imesaidia thamani yake kuongezeka kwa asilimia 243 - sawa na Pauni 10.4 milioni.

Chanzo: Mwanaspoti