Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za usajili Bongo

Aziz KI X Guede X Dube Tetesi za usajili Bongo

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imepanga kuachana na nyota wao Kennedy Musonda na Augustine Okrah kuelekea msimu ujao.

Deal done; Nizar Khalfan amesaini mkataba wa kuwa kocha msaidizi wa Mecky Maxime katika klabu ya Dodoma Jiji.

Stephen Aziz Ki amekubali kusaini Mkataba mpya wa mwaka mmoja, ndani ya Yanga Sc.

Klabu ya Simba iko katika hatua za mwisho kumsainisha mkataba mchezaji Kelvin Kapumbu (28) raia wa Zambia anayecheza klabu ya Zesco United. Huu utakuwa usajili wa pili baada ya Joshua Mutale unaosimamiwa na Crescentius Magori aliyekwenda nchini Zambia kuwanasa nyota hao.

Nyota wa klabu ya Yanga Sc Djigui Diara amedai kuongezewa dau kwenye Mkataba wake wa sasa na viongozi wamekubali.

Kiungo mkabaji wa klabu ya Yanga Zawadi Mauya ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Yanga

Baada ya dili la Joshua Mutale kwenda vizuri kwa Mnyama (Almost Deal Done) Sasa Simba wanahitaji saini ya Mchezaji wa Madeama ????????Fordjour (21), Derrick Fordjour bado anao mkataba wa mwaka mmoja na nusu na waajiri wake Madeama. According to Transfermarkt Fordjour anathamani ya €125k sawa na 350,866,031.

Taarifa za ndani kabisa zinadai kuwa rais wa heshima wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji amemwalika mlinda mlango wa timu hiyo Ayoub Lakred nyumbani kwake huko Dubai ili kumaliza michakato ya kuongeza mkataba, Mkataba wa nyota huyo unamalizika June 30 mwaka huu na kumekuwa na mazungumzo baina ya nyota huyo na klabu ambayo hayajafikiwa mwafaka na inaelezwa kuwa Lakred anataka dau la Tsh million 500 ili asaini kandarasi mpya.

Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa beki wa kushoto wa FC Lupopo, Chadrac Boka mwenye miaka 24,ni mbadala wa Lomalisa Mutambala ambaye atatimka mwisho wa huu msimu, huyu beki huko DR Congo wanamuita Rais wa Maji au Marcelo wa DR Congo.

Kuelekea msimu ujao klabu ya Mashujaa wameonesha nia ya kuhitaji saini ya winga Kinda wa Yanga Denis Nkane ambae wanaona anaweza kwenda kuwa nyongeza nzuri kwenye kikosi chao

Klabu ya Simba Iko katika mazungumzo na kiungo mshambuliaji Sou D'Avila kutoka katika klabu ya LYS Sassandra ya ligi kuu nchini Ivory Coast ili aje kuwatumikia msimu ujao.

Klabu ya Amani Queens imeaga rasmi katika mkoa wa Lindi baada ya kuibamiza Baobab Queens na kuishusha daraja huku ikielezwa kuwa timu hiyo imeuzwa Kwa jeshi la wananchi JWTZ linalomiliki timu ya Mashujaa FC ya mkoani Kigoma.

Timu hiyo kuanzia msimu ujao wa ligi kuu ya wanawake Tanzania itajulikana kama Mashujaa Queens na itatumia uwanja wa lake Tanganyika mkoani Kigoma ambapo itakuwa makao yao mapya.

Kiungo mkabaji Yusufu Kagoma amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba akitokea Singida Fountain Gate FC.

Mangungu "Pesa za usajiri niko tayari kutoa mwenyewe kwa kushirikiana na wanachama na wapenzi wa Simba, kwa sasa natafuta Mkurugenzi wa ufundi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia mtandao wa usajili na upembuzi wa kina kabla ya mchezaji kusajiliwa.”

Rasmi Philippe Kinzumbi amesajiliwa kama mchezaji mpya wa Raja Club kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DRC. Sasa ni rasmi klabu ya Yanga imemkosa winga huyo baada ya kushindwana na klabu yake ya TP Mazembe.

Metacha Mnata amejiunga na klabu ya singida Black stars zamani ilifahamika Kama Ihefu akitokea klabu ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live