Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Ulaya 25.10.2021: Perisic, Ten Hag, Fulgini, Marcelo, Rice, Diaz, Ndombele

Marcelo Mlinzi wa Real Madrid, Marcelo

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: BBC Sports

Beki wa kushoto Mbrazili Marcelo, 33 ameiambia Real Madrid kwamba ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huku huenda akatua katika klabu ya Fluminese ya nyumbani Brazil. (El Nacional - in Catalan)

Klabu za Everton na West Ham ni miongoni mwa vilabu vinavyomuwania winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 32. Hata hivyo vilabu vya ligi kuu ya Ujerumani ' Bundesliga'' vimeonyesha pia nia za kumtaka Mcroatia huyo. (Fichajes - in Spanish)

Newcastle United itapaswa kuweka mezani ofa ya kipekee na isiyo ya kawaida kumpata bosi wa Ajax Erik ten Hag ili awe Kocha wao mpya. (Chronicle Live)

Kiungo wa Angers Angelo Fulgini anavivutia vilabu vya ligi kuu England baada ya mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 25 kufunga goli dhidi ya Paris St-Germain mwishoni mwa juma lililopita. (Sun)

Kocha wa West Ham David Moyes ameonya kwamba klabu yoyote inapaswa kulipa kitita kinene cha zaidi ya Pauni milioni 100 ili kumsajili kiungo wa England Declan Rice. (Sky Sports via Manchester Evening News)

Chelsea imeulizia kuhusu upatikanaji wa winga Luis Diaz lakini klabu za Newcastle, Bayern Munich na Real Madrid pia zimewasiliana na wawakilishi wa winga huyo mwenye miaka 24. (Nicolo Schira on Twitter)

Kiungo mfaransa Tanguy Ndombele, 24, anasema kikao cha mgogoro na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy kiliokoa maisha yake ya soka pale Tottenham Hotspurs. (Sun)

Mazungumzo kati ya Paul Pogba, 28 na Manchester United kuhusu mfaransa huyo kusaini mkataba mpya yamesimamishwa mpaka mwezi April na wakala wake Mino Raiola. (AS - in Spanish)

AC Milan na kiungo Franck Kassie,24 wanaendelea kusuaga kuhusu mkataba mpya huku Muivorycost huyo akiendelea kuhusishwa na vilabu kadhaa barani Ulaya. (Calcio Mercato - in Italian)

Mlinzi wa kati wa Chelsea Antonio Rudiger anatajwa kutaka kuondoka Stamford Bridge msimu ujao huku Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 28 akihusishwa na vilabu vya Juventus, Manchester City, Tottenham na Paris St-Germain. (Wettfreunde - in German)

Chanzo: BBC Sports