Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Ulaya 24.10.2021: Coady, Pogba, Overmars, Tielemans, Pepi, Dybala, Kroos, Kounde

Conor Coady Conor Coady

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: BBC Sports

Nahodha wa Wolves Conor Coady yuko kwenye orodha ya wanaowaniwa na klabu ya Newcastle United katika dirisha dogo la Januari huku ada ya mlinzi huyo wa England mwenye miaka 28 ikitajwa kuwa kama Pauni milioni 20. (Sun)

Mchezaji wa zamani wa Uholanzi Marc Overmars ameanza mazungumzo na Newcastle ili kuwa mkurugenzi wao mpya wa masuala ya soka. (Mirror)

Manchester United watafanya kila wawezalo ili kumbakiza kiungo mfaransa Paul Pogba Old Trafford huku Real Madrid ikiwa na matumaini ya kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 mwishoni mwa msimu. (AS - in Spanish)

Meneja wa timu ya taifa ya Ubelgiji Robert Martinez amekataa ripoti kwamba kiungo wa Ubelgiji Youri Tielemans amekataa mkataba mpya Leicester City huku nyota huyo mwenye miaka 25 akivivutia vilabu kadhaa zikiwemo Liverpool na Manchester United. (Mail) mm

Mshambuliaji kinda wa FC Dallas Ricardo Pepi anavivutia vilabu kadhaa vya Ligi kuu England huku Liverpool na Manchester United vikiwa miongoni mwa vilabu vilivyonyesha nia ya kumtaka nyota huyo kutoka Amerika mwenye miaka 18. (Mirror)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Paulo Dybala, 27, amefikia muafaka kusaini mkataba mpya wakati wowote kusalia Juventus. (Calciomercato - in Italian

Chelsea imeonywa na Sevilla kwamba hawamuuzi kwa bei chee mlinzi wake wa kifaransa Jules Kounde, 22. (Sun)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anamfuatilia kiungo wa Real Madrid Toni Kroos huku mkataba wa sasa wa mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 31 ukimalizika mwaka 2023. (El Nacional - in Catalan)

Everton wanaongoza mbio za kumsajili Jesse Lingard kutoka Manchester United lakini kiungo huyo muingereza mwenye umri wa miaka 28 anasakwa pia na vilabu vya West Ham and Newcastle. (Football Inside)

Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Urguay Luis Suarez anataka kuendelea kusalia klabuni hapo hata baada ya msimu huu. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 amefunga mabao 5 msimu huu lakini mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu ujao. (Marca - in Spanish)

Ajax wanataka kumbakiza kiungo wake mholanzi Ryan Gravenberch, ambaye anavivutia vilabu kadhaa vikubwa vikiwemo Liverpool, Manchester United, Barcelona na Juventus, na sasa wanataka kumpa mkataba mpya kinda huyo mwenye miaka 19. (Fichajes - in Spanish)

Chanzo: BBC Sports