Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Ulaya 17.10.2021: Salah, Hazard, Haaland, Jovic, Lacazette, Kounde

Salahhhh Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah

Sun, 17 Oct 2021 Chanzo: BBC Sports

Real Madrid watamuuza kiungo wao Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 30, ili kupata pesa kwa ajili ya mshambuliaji wa Liverpool Mmisri, Mohamed Salah,mwenye umri wa miaka 29. (Ekrem Konur)

Wakala wa Salah amesafiri hadi Liverpool kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya ana kwa ana kuhusu mkataba mpya. (Mirror, via Star Online)

Newcastle United wanamsaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, huku Real Madrid,Manchester City na Paris St-Germain wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway. (AS, via Sport Witness)

Newcastle wamepanga bajeti ya pauni milioni 50 tu kwa ajili ya dirisha la kwanza la uhamisho chini ya wamilikiwao wapya Wasaudia . (Sunday Telegraph)

Manchester United imetenga kando pauni milini 70 kwa ajili ya dirisha lijalo la uhamisho, ambazo zitatumika ilimradi wanahisi kuwa wanaweza kupata taji la Primia Ligi. (Star Sunday)

Mshambuliaji wa Real Madrid Mserbia Luka Jovic, 23, anatzamiwa kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette, 30, katika kikosi cha Arsenal. (Fichajes)

Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Jack Wilshere, 29, amemshauri mlinzi wa England Declan Rice, 22, akatae ofa za uhamisho kutoka Manchester United na Chelsea na aendelee kubakia West Ham. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Arsenal na nahodha wa Norway Martin Odegaard, mwenye umri wa miaka 22, yuko tayari kupokea wazo la kurejea katika klabu ya Real Sociedad, anasema mlinda mlango wa zamani wa Gunners Maustralia Mat Ryan, 29, ambaye kwa sasa yuko Real Sociedad. (Mundo Deportivo, via Mirror Online)

Wakala wa Robert Lewandowski anasema kuwa Manchester City ndio "timu anayoweza kuhamia" mshambuliaji huyo wa Poland na Bayern Munich mwenye umri wa mika 33, siku zijazo. (Bild, via Star Online)

Mlinzi wa klabu ya Sevilla Jules Kounde amemuomba wakala wake kufanya mazungumzo na Manchester United, huku mchezaji huyu wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 pia akilengwa klabu za Chelsea na Real Madrid. (El Nacional - in Spanish)

Mlinzi wa zamani wa Barcelona Dani Alves amejitolea kujiunga tena na klabu hiyo kwa mkataba wa 'garama ya chini'. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 38 sasa yuko hurubaada ya kusitisha mkataba wake na Sao Paolo katika mwezi wa Septemba. (AS - in Spanish)

Mchezaji wa safu ya ulinzi wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, mwenye umri wa miaka 28, anataka malipo ya pauni 400,000 kwa wiki ili asaini mkataba mpya katika Stamford Bridge. (MailOnline)

Liverpool wamejiunga katika mbio za kumsaka mshambuliaji wa Club Bruges na Uholanzi mwenye umri wa miaka 22, Noa Lang sambamba na Arsenal na Leeds. (Calciomercato, via Teamtalk)

Huenda Chelsea imebadilisha uamuzi wake wa kumuondoa kikosini kiungo wa kati wa Scotland Billy Gilmour, 20, ambaye kwa sasa mkataba wake umemalizika Norwich baada ya meneja wa Canaries Daniel Farke kusema kuwa "Hatuko hapa kuwakuza wachezaji kwa ajili ya klabu nyingine ". (Express Online)

Kiungo wa kati wa Rangers Joe Aribo, 25, ananyatiwa na Crystal Palace. (Football Insider)

Beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher anasema pesa sio dhamana ya kufanikiwa na atashangaa Newcastle ikichukua taji la Ligi Kuu kabla ya 2030. (Telegraph - subscription required)

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, hatasaini mkataba mpya Paris St-Germain haijalishi klabu hiyo ya Ligue 1 itamlipa kiwango gani cha fedha kwani nyota huyo ameamua kuelekea Real Madrid. (AS - in Spanish)

Liverpool, Manchester City na Manchester United awanamnyatia kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 21, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa karibu £40m. (ESPN)

Manchester City wanapanga kujaza pengo litakaloachwa na mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26, na mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33. (Express)

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekubali kuwa kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28, huenda asishawishike kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo mpaka apatiwe muda zaidi wa kucheza. (Evening Standard)

Wakala wa Paul Pogba, Mino Raiola amemtoa kiungo huyo wa kati wa Manchester United kwa Barcelona. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa wa miaka 28- katika uga wa Old Trafford unatarajiwa kumalizika msimu ujao na Raiola amewasiliana na Juventus, Paris St-Germain, Real Madrid klabu zingine kadhaa za Ligi ya Primia. (ESPN)

Chanzo: BBC Sports