Tetesi za soka Ulaya 16.11.2021: Salah, Azpilicueta, Sterling, Tchouameni, Lacazette, Lingard, Kounde
Barcelona "inafanyia kazi kimya kimya" mpango wa kumvuta mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah kumleta Nou Camp, huku meneja mpya Xavi akimtaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 "kwa gharama zozote". (El Nacional - in Catalan)
Barca wanafuatilia pia suala la Cesar Azpilicueta, 32 pale Chelsea. Mlinzi huyo Mhispania, 32, yuko katika miezi 8 ya mwisho ya mkataba wake pale Chelsea. Klabu hiyo ya Hispania inalenga kusajili zaidi wachezaji huru ama wasiokuwa na mikataba kutokana na hali yake ngumu kifedha. (ESPN)
Mpango wa Barca wa kumsajili kwa mkopo winga wa England Raheem Sterling kutoka Manchester City mwezi Januari "unaonekana kama sio rahisi" kwa sababu ya hali yao kifedha na mshahara wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 26.
Juventus wanataka kumuondoa winga wake raia wa Sweden Dejan Kulusevski, 21 huku kukipendekezwa mpango wa kubadilishana na Arsenal ili wamchukue winga wao kutoka Ivory Coast Nicolas Pepe, 26, klabu hiyo ya Italia inataka fedha taslimu. (Calciomercato - in Italian)
Newcastle United inamtaka kiungo wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 21, ambaye pia anasakwa na vilabu vya Chelsea, Liverpool na Manchester City pamoja na Real Madrid, Paris St-Germain na Bayern Munich. (El Nacional, via Sun)
Aston Villa wanamtaka mlinzi wa Rangers Nathan Patterson kufuatia ujio wa Steven Gerrard kama kocha wao mpya akitokea kwa mabingwa wa Scotland, Rangers - lakini wanakabiliwa na ushindani mkali kumsajili mlinzi huyo wa kulia raia Scotland mwenye miaka 20, ushindani kutoka vilabu vya Bayern Munich, Atletico Madrid na Paris St-Germain. (90min)
Nuno Espirito Santo anataka kurejea kufundisha haraka katika ligi kuu England baada ya kutimuliwa Tottenham lakini wakala wake anaangalia uwezekano wa kocha huyo kwenda Ufaransa huku timu za Lyon na Lille zikionekana mahali atakapoweza kwenda. (Sun)
Leeds United, Wolves na Burnley wanamnyatia kiungo wa Reading na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 John Swift,26 ambaye kwa muda mrefu anasakwa na Sheffield United. (Sheffield Star)
AC Milan imeungana na Chelsea na Atletico Madrid katika mbio za kumuwania mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa chini ya miaka 17 Mohamed-Ali Cho, 17, kutoka Angers. (L'Equipe - in French)
Mshambuliaji mfaransa Alexandre Lacazette, 30, na mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 Eddie Nketiah, 22, wanajiandaa kutimka Arsenal mikataba yao itakapomalizika katika majira ya joto. (Football London)
Newcastle United wanamatumaini kwamba fursa ya kuanza kikosi cha kwanza kutaongea nafasi yao ya kumsajili kiungo wa England Jesse Lingard, 28, kutoka Manchester United mwezi Januari - huku West Ham ikionyesha nia pia ya kumtaka.(Northern Echo)
Mlinzi wa Uholanzi Stefan de Vrij, 29, amewaambia marafiki zake anataka kuondoka Inter Milan kujiunga na Tottenham mwezi Januari. (Football Insider)
Beki wa kati mfaransa wa Sevilla Jules Kounde, 23, anasema kushindwa kwa Chelsea kumsajili katika majira ya joto kumeathiri kiwango chake msimu huu. (Telefoot, via Goal)
Kiungo wa Senegal Nampalys Mendy, 29, anataka kuondoka Leicester City lakini anasema "anapaswa kuwa na subira" ili kufanikiwa kufanya hivyo. (APS, in French)
Birmingham City imempa mkataba wa kulipwa kiungo wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 18 George Hall, 17, wakitaka kuwaondoa kwenye reli Leeds United wanaomtaka. (Football Insider)
Kocha wa Inter Miami Phil Neville amewaondoa wachezaji 10 kwenye kikosi chake baada ya kushindwa kwenye kwenye Ligi ya Marekani "MLS play-offs" ,mtoto wake Harvey, 19, anatarajiwa kupandishwa kikosi cha kwanza msimu ujao. (Sun)