Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Ulaya 14.11.2021: Lingard, Thiago, Pochettino, Pulisic, Ake, Ndidi, Pogba

 121550230 3a83cc2c 5b9c 4ba5 8d3f 525f7d7d4bcb Jesse Lingard

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: BBC Sports

Manchester United wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Jesse Lingard kwa Pauni miloni 10 mwezi Januari. (Sun)

Meneja mpya wa Barcelona Xavi anataka klabu hiyo kumsajili tena kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara, 30, kutoka Liverpool. (Sport - in Spanish)

Meneja wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino atakaribisha uwezekano wake kurejea kwenye Ligi ya Premia. (Telegraph - subscription required)

Barcelona wanafikiria kumnunua kwa mkopo kiungo wa kati wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 23. (Sport - in Spanish)

Beki wa Manchester City na Uholanzi Nathan Ake, 26, analengwa sana na meneja mpya wa Newcastle Eddie Howe, ambaye hapo awali alikuwa meneja wa Ake huko Bournemouth. (90min)

Kiungo wa kati wa Leicester City na Nigeria Wilfred Ndidi, 24, yuko kwenye rada za Real Madrid. . (Mundo Deportivo - in Spanish)

Real Madrid bado wanamfuatilia kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba mwenye umri wa miaka 28. (Marca - in Spanish)

Chelsea na Real Madrid wanaweza kupambana katika kumnunua mchezaji wa Bayer Leverkusen na mchezaji wa Ujerumani Florian Wirtz, 18. (El Nacional - in Catalan)

Chelsea inaandaa ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 21. (TuttoJuve - in Italian)

Chelsea wametuma dau la pauni milioni 34 kumnunua beki wa Real Madrid na Brazil Eder Militao, 23. (El Nacional - in Catalan)

Roma wanazidisha juhudi za mazungumzo na Manchester United kuhusu mkataba wa mkopo na chaguo la kumnunua beki wa pembeni wa Ureno Diogo Dalot, 22. (Corriere dello Sport, via Football Italia)

Leeds United imefanya mawasiliano na mshambuliaji wa Arsenal na England aliye chini ya umri wa miaka 21 Eddie Nketiah kuhusu kurejea Elland Road. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 hapo awali alitumia miezi sita kwa mkopo na Leeds kabla ya kurejeshwa. (Tuttomercato)

Huku meneja mpya Steven Gerrard akiwa usukani, Aston Villa wanavutiwa na kiungo wa kati wa Rangers na Finland Glen Kamara, 26. (Record)

Gerrard pia anataka kumleta winga wa Rangers Ryan Kent, 25, hadi Villa. (Metro)

Mshambulizi wa Arsenal na England U21 Folarin Balogun, 20, anasema yuko tayari kuhama The Gunners ili kupata soka ya kikosi cha kwanza. . (Mirror)

Chanzo: BBC Sports