Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Ulaya 02.10.2021: Sterling, Vlahovic, Haaland, Werner, Ndombele, Torres, Tuanzebe

Raheem Sterling Mshambuliaji wa England na Manchester City, Raheem Sterling

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: BBC Sports

Winga wa England Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 26, bado anakabiliwa na sintofahamu kuhusu siku zake zijazo katika kikosi cha Manchester City licha ya "makataba usio rahisi " na meneja wa klabu hiyo Pep Guardiola. (Daily Telegraph - subscription required)

Mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia Dusan Vlahovic, mwenye umri wa miaka 21, ana ndoto za za kuhamia katika timu ya Manchester City. Klabu hiyo ya Championi ya Primia Ligi ilihusishwa na uhamisho wa mchezaji huyo katika kipindi cha msimu uliopita (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Thierry Henry amemkosoa mpango wa meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger kwa ajili ya kombe la dunia kila baada ya miaka miwili ambao aliutaja kuwa "unachosha akili". (Sun)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amemwambia winga wa England mwenye umri wa miaka 21 Jadon Sancho kuwa mkweli, wakati akisubiri bao lake la kwanza katika klabu hiyo. (Mirror)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, mwenye umri wa miaka 25, anakabiliana na kupambania hali yake ya baadaye katika klabu hiyo baada ya kuhangaika kuimarika katika klabu hiyo tangu kuwasili kwa Romelu Lukaku. (London Evening Standard)

Manchester City wanaangalia kuwezekano wa kufanya dau na mlinzi wa Villarreal na Uhispania Pau Torres, mwenye umri wa miaka 24. (Marca)

Jose Mourinho anapanga mpango wa kushitukiza wa kukutana tena na shambuliaji wa Tottenham Mfaransa Tanguy Ndombele, 24, katika harakati za kumshawishi ajiunge na Roma. (Calciomercarto via Express)

Huenda Everton wakamnunua kiungo wa kati wa Newcastle Muingereza Sean Longstaff, mwenye umri wa miaka 23. (Independent)

Real Madrid watakuwa na pesa za kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Erling Haaland, mwenhye umri wa maika 21, msimu ujao, huku wakiendelea kuwa na nia ya kumnunua nyota wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 22. (AS - in Spanish)

Mlinzi wa Uingereza Axel Tuanzebe, mwenye umri wa miaka 23, yuko wazi kuufanya mkataba wake wa mkopo ndani ya Aston Villa kutoka Manchester United kuwa wa kudumu. (Birmingham Mail)

Chanzo: BBC Sports