Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Ijumaa 12.11.2021: Sterling, Ndidi, Bale, Kulusevski, Van de Beek

Raheem Sterling Mshambuliaji wa England na Manchester City, Raheem Sterling

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: BBC Sports

Manchester City iko tayari kumuuza mshambuliaji Raheem Sterling na thamani ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England imetajwa kuwa karibia pauni milioni 45. (Metro)

Barcelona inafakiria kumnunua Sterling kwa mkopo ,mwezi Januari lakini pia ina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa RB Leipzig raia wa Uhispania Dani Olmo, 23. (Marca - in Spanish)

Mkufunzi mpya wa Barcelona Xavi atakuwa na chini ya kitita cha euro milioni 10 kutumia ili kuimarisha kikosi chake katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (ESPN)

Newcastle inawalenga wachezaji watatu wa klabu ya Manchester United mwezi Januari - Kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 24, kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28, na kipa raia wa England Dean Henderson, 24. (Mirror)

Real Madrid inamnyatia kiungo wa Leicester na Nigeria Wilfred Ndidi, 24, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Leicestershire Live, via Fichajes)

Tottenham haina mpango wa kumsajili winga wa Wales na Real Madrid Gareth Bale, licha ya kuhusishwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 na kurudi kwake katika klabu hiyo ya north London. (Football London)

Spurs ina nia ya kumsaini winga wa Juventus na Sweden mwenye umri wa miaka 21 Dejan Kulusevski. (Calciomercato - in Italian) Gareth Bale

Arsenal pia inamtazama Kulusevski, ambaye amekuwa hachezeshwi katika klabu ya Juventus msimu huu. (Sky Italy - in Italian)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Matteo Guendouzi, 22, anataka kusalia katika klabu ya Marseille wakati mkopo wake kutoka Arsenal utakapoisha katika klabu hiyo . (RMC, via Mirror)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 33, ameambiwa kuipatia kipau mbele kandanda badala ya maslahi ya matangazo na rais wa klabu ya Fenerbahce Ali Koc.

Barcelona haitamsajili upya beki wa kulia wa Brazil Dani Alves, ambaye ni mchezaji huru na amehusishwa na klabu hiyo. (Goal)

Arsenal ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa RB Leipzig na Marekani Tyler Adams, 22. (Mirror, via Sport Bild)

Beki wa kati wa klabu ya Fenerbahce mwenye umri wa miaka 23-raia wa Hungary Attila Szalai ananyatiwa na Chelsea pamoja na Atletico Madrid. (CNN Turk, in Turkish)

Chanzo: BBC Sports