Manchester United wanaamini kuwasili kwa Ralf Rangnick Old Trafford kutawapa faida katika haakati zao za kumsajili Erling Haaland,21, wa Borussia Dortmund majira yajayo ya joto. (Mirror)
Kocha wa West Ham David Moyes anajiandaa na karata yake ya mwisho kumsajili mlinzi wa Burnley James Tarkowski huku mchezaji huyo akitarajiwa kuwa mchezaji huru. (Sun)
Fiorentina wameweka bei ya pauni milioni 55 ya kumnunua mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic kwa nia ya kusimamisha nia ya Manchester United - lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 hatarajiwi kuhama mwezi Januari. (Mail)
Mchezaji wa Arsenal Alexandre Lacazette amesema kuwa mawakala wake wanafikiria wapi atakwenda huku kandarasi ya mshambuliaji huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 30 ikikamilika msimu wa joto. (Telefoot via Athletic)
Real Madrid hawatamsajili kiungo wa kati wa Manchester United, Paul Pogba msimu ujao wa joto ingawa klabu hiyo imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa na mpango wa kumnasa mchezaji huyo, 28. (Marca-in Spanish)
Paris St-Germain hawana mpango wa kumuachia Mauricio Pochettino kwenda Manchester United katikati ya msimu huu, lakini wako tayari kwa mazungumzo mwishoni mwa msimu. (Goal)
Kiungo mchezeshaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 29, anaweza kuhamia Newcastle katika dirisha la uhamisho wa Januari - ingawa Mbrazili huyo alikataa kuhamia klabu hiyo ya Premier League. (El Nacional)
Pep Guardiola anasema Manchester City itakuwa klabu pekee ya Uingereza atakayoinoa.(Manchester Evening News)
Mshambuliaji wa Ufaransa Nabil Fekir, 28, yuko mbioni kufanya makubaliano na Real Betis kuhusu mkataba mpya. (Mundo Deportivo-in Spanish)
Crystal Palace wanamfuatilia mshambuliaji wa Kihispania Borja Mayoral huku mchezaji huyo mwenye miaka 24 akipambana kupata nafasi ya kucheza akiwa kwa mkopo Roma akitokea Real Madrid. (Sun)
Arsenal na Tottenham zote ziko kwenye ushindani wa kumsajili kiungo wa kati wa Sweden Dejan Kulusevski mwenye umri wa miaka 21 kutoka Juventus.(Calcio Mercato-in Italian)
Mtendaji mkuu wa Aston Villa Christian Purslow anasema kunaweza kuwa na mchezaji "mmoja au wawili" watakaoingia Villa Park wakati wa dirisha la usajili la Januari. (Birmingham Mail)