Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Barani Ulaya, Novemba 18

Haaland Haaland Mshambuliaji wa Dortmund, Erling Braut Haaland

Thu, 18 Nov 2021 Chanzo: BBC Sports

Klabu za Manchester United na Chelsea zimepata nguvu zaidi za kumshawishi mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland, ambaye mkataba wake utamruhusu kuondoka kwa ada ya Pauni milioni 64 msimu ujao, huku Real Madrid ikikiri nyota huyo Mnorway mwenye miaka 21 ataelekea ligi kuu ya England. (Sun)

Au Real Madrid inapanga kutunishiana misuli na vilabu vya Chelsea, Manchester City na Paris St-Germain kwa kumuongeza Haaland na mshambuliaji mfaransa wa PSG Kylian Mbappe, 22, kwenye safu ya ushambuliaji ambayo tayari ina Mbrazil Vinicius Junior, 21. (AS - in Spanish)

Newcastle United wanapanga kumsajili mlinzi mholanzi Stefan de Vrij, 29, na kiungo wa Croatia Marcelo Brozovic, 28, kutoka Inter Milan mwezi Januari, pamoja na kipa wa Lazio Mualbania Thomas Strakosha mwenye miaka 26. (Times)

Wakala wa Paul Pogba amegusia kwamba kiungo huyo mfaransa mwenye umri wa miaka 28 ataondoka Manchester United mwezi Januari, kabla mkataba wake kumalizika majira ya kiangazi. (Rai, via Goal)

Manchester United inajiandaa kupambana na Barcelona kwa ajili ya kumsajili winga mhispania wa RB Leipzig Dani Olmo, 23. (El Nacional - in Catalan)

Mlinzi wa Kijerumani Antonio Rudiger, 28, amekua akikasirishwa na ofa ya mkataba wa hivi karibuni Chelsea, ambao haukidhi matakwa yake, kuna upungufu ama tofauti ya kiasi cha Puni elfu 60,000 cha mshahara anaotaka kwa wiki. (Bild, via Sun)

Arsenal wako tayari kumpa mkataba mfupi mshambuliaji wake mfaransa Alexandre Lacazette,30 ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu. (Athletic, via Sun)

Villarreal wanapanga kugomea ofa zote zinazotakwa kumsajili winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma mwezi Januari huku Liverpool ikimfuatilia mshambuliaji huyo wa zamani Bournemouth mwenye miaka 24. (Football Insider)

Manchester United imeanza mpango wake wa kuleta mbadala wa kocha Ole Gunnar Solskjaer, huku chaguo lao kubwa ni kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers. (Manchester Evening News)

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane amejibu ombi la Manchester United kwa kusema atapatikana mwishoni mwa msimu. (Bild, via Express)

Kocha mpya wa Barcelona Xavi anataka kumbakiza mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele lakini imemtaarifu nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 kwamba "ni sasa ama kamwe" kwa yeye kusaini wakati huu mkataba wake ukielekea mwisho. (AS - in Spanish)

Rais wa Barca Joan Laporta "hatapinga" uwezekano wa mshambuliaji wa Paris St-Germain Lionel Messi, 34 na kiungo wa Vissel Kobe Andres Iniesta, 37, kumfuata nyota mwenzao wa zamani Dani Alves kurejea klabuni hapo. (Marca - in Spanish)

Frank Lampard alifanyiwa usaili kwa ajili ya kuwa kocha wa Aston Villa lakini mchezaji mwenzake wa zamani wa timu ya taifa ya England, Steven Gerrard, ambaye alirithi mikoba ya Dean Smith wiki iliyopita, alikua anaonekana chaguo pendwa. (Sun)

Nahodha wa timu ya vijana ya England chini ya miaka 18 Sammy Braybrooke atasaini mkataba wa kulipwa pale Leicester City licha ya vilabu vya Ujerumani kuonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 17. (Athletic, via Leicester Mercury)

Chanzo: BBC Sports