Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Barani Ulaya, Disemba 6

Mohamed Salah.jpeg Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: BBC Sports

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe haajamuwa iwapo hatoendelea kuwa katika Paris St-Germain, ambao walikataa ofa kutoka Real Madrid kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 katika msimu wa kiangazi. Mkataba wa Mbappe na PSG unamalizika msimu huu. (Amazon Prime, via Goal)

Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Fabian Ruiz analegwa na Liverpool, ambao wanataka kumuingiza kikosini kiungo huyo wa kati wa Napoli mwenye umri wa miaka 25 msimu ujao. (Fichajes.net)

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, 29, amerejelea tena kauli yake kwamba anataka kuendelea kubaki katika klabu hiyo lakini "uamuzi uko mikononi mwa utawala wa klabu na ni lazima watatue suala hili". Mkataba wa Mshambuliaji huyo Mmisri unakwisha katika msimu wa kiangazi mwaka 2023 na anafanya mazungumzo kuhusu mkataba wake mpya. (MBC Masr TV, via Liverpool Echo)

Meneja wa Ajax Erik ten Hag amehusishwa na taarifa za kuchukua umeneja katika Klabu ya Manchester United na Mholanzi huyo anasema yuko tayari licha ya "changamoto" ya kuwa meneja wa klabu ya ugenini. (De Volkskrant, via Mirror)

Barcelona watamuomba winga Mfaransa Ousmane Dembele kuwaambia iwapo atasaini nao mkataba mpya kufikia tarehe 31, huku mkataba na mchezaji huyo mweye umri wa miaka 24 ukimalizika msimu huu. (Sport - in Spanish)

Mshamhuliaji Mbelgiji Dries Mertens anasema anatumai Napoli watachagua kurefusha mkataba wake kwa ajili ya msimu mwingine, Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ukitarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu ujao. (Sky Sports Italia - in Italian)

Southampton wanaangalia uwezekano wa kumhamisha Mlinda lango wa Argentina kwenye umri wa miaka Willy Caballero, ambaye ni wakala huru baada ya kuondoka Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita. (Talksport)

Mmiliki mwenza wa klabu ya Newcastle United Mehrdad Ghodoussi amekataa madai kwamba klabu hiyo ilimpatia kazi Michael Emenalo ya mkurugenzi wa soka au mkurugenzi wa michezo baada ya kukataa kazi hizo. (Star)

Leeds United wamekubali dili la Espanyol katika kumsainisha mshambuliaji Mateo Joseph Fernandez kutoka Spanish club.

Nyota huyo mwenye miaka 18 amezaliwa Uhispania, lakini bado anavibali vya kuwa muingereza na hiyo ni kutokana na wazazi wake. (Mail on Sunday)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema kuwa yupo tayari kusaidiana na mchezaji wa zamani wa Manchester City raia wa Ivory Coast Yaya Toure ili ainoe pamoja nae kwenye timu hiyo, Toure, 38, kwasasa yupo kwenye klabu ya Tottenham. (Sunday Mirror)

Winga wa Southampton na Norway Mohamed Elyounoussi, 27, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal na Leicester City, anasema kuwa familia yake sasa imetulia katika klabu hiyo ya mwambao wa kusini. (Hampshire Live)

Chanzo: BBC Sports