Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Barani Ulaya, Disemba 5

Lingard Jesse Lingard

Sun, 5 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Newcastle United imeanza kuonesha nia ya kumtaka kiungo wa Uingereza Jesse Lingard katika dirisha dogo la Januari, mchezaji huyo mwenye miaka 28 kandarasi yake inataraji kuisha katika kipindi cha kiangazi. (Times - subscription required)

Mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Chelsea Michael Emenalo ameitupilia mbali ofa ya kuwa mkurugenzi wa mpira ndani ya Newcastle.(Sunday Telegraph - subscription required)

Huenda Everton ikamchukua kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho ambaye kwasasa anainoa Roma, maamuzi hayo yatafanyika mpaka waanze mchakato wa kumuondoa kocha wa sasa Rafael Benitez. (Daily Star on Sunday)

Kiongozi mkuu wa Borussia Dortmund Michael Zorc amemruhusu nyota wa Norway straika Erling Braut Haaland 21, tetesi zinasema kuwa teyari £75m zimewekwa mezani, na mchezaji yupo mbioni kuondoka klabuni hapo. (Sunday Mirror)

Barcelona imeonesha nia ya kumpatia ofa nono winga Ousmane Dembele 24, kiungo wa nyuma wa Ufaransa Samuel Umtiti 28, M'Brazil Philippe Coutinho, 29, kiungo mkabaji Mfaransa Clement Lenglet, 26 , Mhispania Ferran Torres, 21, kutoka Manchester City, Ila bado haijathibitishwa kama timu zao zipo tayari kuwaachia (Marca - in Spanish)

Tottenham imeungana na Manchester United pamoja na Newcastle United katika kuitaka saini ya Dembele, mchezaji huyo ambaye mkataba wake na Barcelona unaelekea ukingoni katika kipindi cha kiangazi.(Mundo Deportivo - in Spanish)

Klabu ya nchini Italia,Juventus nayo imeanza mchakato wa kuitaka kandarasi ya nyota wa Barcelona Dembele, lakini pia Paris St-Germain imeonesha utayari wa kumchukua mchezaji huyo. (Sport - in Spanish)

Umtiti ni mmoja wa wachezaji aliorodheshwa na AC Milan, timu hiyo ambayo safu yake ya ulinzi imekuwa ikitetereka kutokana na mchezaji raia wa Denmark Simon Kjaer, 32 kuwa majeruhi kwa muda mrefu. (Sport - in Spanish)

Arsenal na Totttenham wameonesha utayari wao wa kutaka kumchukua kiungo wa kati wa Juventus Dejan Kulusevski, 21,huku wakimtaka kwa mkopo raia huyo wa Sweden (Calciomercato, via Football Italia)

Leeds United wamekubali dili la Espanyol katika kumsainisha mshambuliaji Mateo Joseph Fernandez kutoka Spanish club.

Nyota huyo mwenye miaka 18 amezaliwa Uhispania, lakini bado anavibali vya kuwa muingereza na hiyo ni kutokana na wazazi wake. (Mail on Sunday)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema kuwa yupo tayari kusaidiana na kocha wa zamini wa Manchester City raia wa Coast Yaya Toure ili ainoe pamoja nae kwenye timu hiyo, Toure, 38, kwasasa yupo kwenye klabu ya Tottenham. (Sunday Mirror)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live