Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Barani Ulaya, Disemba 4

Acf Fiorentina V Spezia Calcio Serie A Scaled E1638446007745 Dusan Vlahovic

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: BBC Sports

Manchester City wanamfuatilia mshambuliaji wa Fiorentina MSerbia Dusan Vlahovic. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amefungia mabao 19 klabu na taifa msimu huu. (La Repubblica)

Maafisa wa Barcelona wamefanya mazungumzo na Manchester City kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Ferran Torres, 21, mwezi Januari. Torres amefunga mabao tisa na kutoa asisti tatu katika mechi 28 za ligi ya primia kwa City. (ESPN)

Hatahivyo, Rais wa Barca Joan Laporta amesema hali ya kifedha ya klabu hiyo ina maana kuwa hawawezi kufanya usajili.(Marca)

Mwenyekiti wa Everton Bill Kenwright ameitisha kikao cha dharura cha bodi, huku mustakabali wa kocha Rafael Benitez ukitarajiwa kujadiliwa. (Mirror)

Liverpool wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Lille na Ureno Renato Sanches, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa Pauni milioni 34.(Fichajes-in Spanish)

Mshambulizi wa Lille raia wa Canada, Jonathan David, 21, yuko kwenye rada za Arsenal. The Gunners wamekuwa wakihusishwa na mshambuliaji wa Everton wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin lakini David - mfungaji bora wa Ligue 1 - pia analingana ana sifa ambazo Gunners wanatafuta. (London Evening Standard)

Everton wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Zenit St Petersburg na Iran Sardar Azmoun, 26, ambaye hapo awali amekuwa akihusishwa na West Ham, Tottenham na Arsenal.(90min)

Kiungo wa kati wa Inter Milan na Denmark Christian Eriksen, 29, anakaribia kukatiza kandarasi yake. Eriksen hajacheza tangu alipopatwa na mshtuko wa moyo kwenye Euro 2020. (calciomercato.com)

Real Madrid wana hakika kuwa watamsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain Mfaransa Kylian Mbappe, 22, ambaye kandarasi yake itakamilika msimu ujao. (AS)

Wakati huo huo, Real iko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Isco, 29, ambaye ameshinda Ligi ya Mabingwa mara nne katika kipindi cha miaka minane katika klabu hiyo. (dakika 90)

Manchester United wanaweza kumuomba kocha wa Austria wa New York Red Bulls Gerhard Struber kuwa msaidizi wa Ralf Rangnick. Wawili hao walifanya kazi pamoja katika klabu ya Red Bull Salzburg.(Sun)

Kiungo wa kati wa Aston Villa na England Carney Chukwuemeka, 18, anahitaji kuwa "mkweli" na kusalia katika klabu hiyo, anasema mlinzi wa zamani wa Uingereza Danny Mills. Chukwuemeka amecheza mechi nne za Ligi ya Primia lakini anaripotiwa kuchoshwa na kukosa nafasi ya kucheza. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 24, hataondoka mwezi Januari. De Jong amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa ikiwemo Manchester City. (Sky Sport Italia)

Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe anasema mshambuliaji wa Kiingereza Dwight Gayle, 32, yuko kwenye mipango yake baada ya mchezaji huyo kuhusishwa na kurejea katika klabu ya West Brom, ambapo alifunga mabao 24 alipocheza kwa mkopo msimu wa mwaka 2018-19. (Birmingham Live)

Chanzo: BBC Sports