Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka Barani Ulaya, Disemba 3

Edinson Cavani.jpeg?fit=736%2C485&ssl=1 Mshambuliaji wa Man United, Edson Cavani

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: BBC Sports

Mshambuliaji wa Manchester United na Uruguay Edinson Cavani, 34, anataka kujiunga na Barcelona msimu ujao wa joto. (Times - subscription required)

Newcastle inawalenga wachezaji wanne wa England mwezi Januari, miongoni mwao kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard, 28, kiungo wa kati wa Tottenham Harry Winks, 25, kiungo wa kati wa Chelsea Ross Barkley, 27, na beki wa Atletico Madrid Kieran Trippier, 31. (Telegraph)

Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, 24, kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette, 30. (Mirror

Beki wa Manchester United na Brazil Alex Telles, 28, ananyatiwa na Inter na AC Milan. (Sun)

Arsenal wanapambana na Juventus katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21, kutoka Fiorentina. (Tuttosport - in Italian)

Borussia Dortmund wamekataa kuthibitisha ikiwa mkataba wa mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21, una kipengele cha kumruhusu kuondoka cha thamani ya kati ya euro milioni 75 na milioni 100.(Sport 1)

Mipango imewekwa kwa Pep Guardiola kuwa mkufunzi wa New York City FC wakati mkataba wake na Manchester City utakapomalizika 2023. (90min)

Liverpool imehusishwa na uhamishio wa winga wa Porto na Colombia Luis Diaz, 24. (Marca)

Mkufunzi mpya wa Tottenham Antonio Conte anataka kuchukua udhibiti kamili wa mchakato wa kuwasajili wachezaji mwezi Januari kwa ushirikiano na mkurugenzi wa mkuu Fabio Paratici. (Football Insider)

West Ham wanataka kumsajili mlinzi wa Manchester City na Uholanzi Nathan Ake, 26. (90min)

Mshambuliaji wa Uhispania Ferran Torres, 21, ameomba kuondoka Manchester City na amefikia mkataba wa miaka mitano na Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kiungo wa kati wa zamani wa Uhispania Isco, 29, ataondoka Real Madrid mwezi Januari ikiwa ofa itakayopokelewa itafaidisha pande zote mbili. (AS - in Spanish)

Beki wa zamani wa Brighton Connor Goldson, 28, amekata kurefushiwa mkataba katika klabu ya Rangers kwa Muingereza huyo ana matumaini ya kurejea katika Ligi ya Primia ifikapo Januari . (Football Insider)

Middlesbrough ni miongoni mwa klabu zinazopania kumsajili mshambuliaji wa England wa chini ya miaka -21 Folarin Balogun, 20, kwa mkopo kutoka Arsenal mwezi Januari. (Standard)

Chanzo: BBC Sports