Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za soka 23.10.2021: Conte, Fonseca, Sanchez, Van de Beek, Saul, Fofana, Rudiger

Conte Inter Antonio Conte

Sat, 23 Oct 2021 Chanzo: BBC Sports

Meneja wa zamani wa Juventus, Chelsea na Inter Milan Antonio Conte "atapenda" kuchukua usukani ndani ya Manchester United iwapo klabu hiyo ya Primia Ligi itamfuta kazi Ole Gunnar Solskjaer. (The Transfer Window Podcast via Star)

Meneja wa zamani wa Roma Paulo Fonseca, mwenenye umri wa miaka 48, yuko tayari kuteuliwa na Newcastle kama meneja baada ya meneja wa zamani wa Chelsea Frank Lampard kujiondoa katika mbio za kuchukua nafasi ya Steve Bruce katika St James' Park. (Mirror)

Everton wanajiandaa kufanya uhamisho kwa ajili ya mshambuliaji wa Inter Milan na Chile Alexis Sanchez, 32, huku mshambuliaji huyo wa zamani Arsenal na Manchester United akiwa huru kuondoka katika klabu ya Italia katika mwezi wa Januari. (InterLive - in Italian)

Chelsea haitatekeleza azimio lake la awali la kusaini mkataba wa kudumu wa pauni milioni 34 na kiungo wa kati wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26, Saul Niguez. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alihangaika kupata mafanikio ya kimchezo tangu alipojiunga na the Blues kwa mkataba wa mkopo katika mwezi wa Agosti. (La Razon - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Uholanzi Donny van de Beek, 24, amemuomba wakala wake kupata uhamisho wake wa kuhamia Real Madrid. (Sun)

Mlinzi Muingereza Chris Smalling, 31, anaweza kuwa mmoja wa wachezaji watakaoondoka Roma katika mwezi wa Julai. (Calciomercato - in Italian)

Mshambuliaji wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo, 36, 'aliharibiwa' na 'kuvunja sheria za usawa na unyenyekevu' katika Juventus. (Mail)

Real Madrid Bayern Munich wanaamini kabisa kuwa watasaini mkataba na kiungo wa safu ya kati-nyuma Mjerumani Antonio Rudiger, mweney umri wa miaka 28 ambaye mazungumzo kuhusu mkataba wake na Chelsea yamefikia kiwango cha kukwama. (ESPN) Getty

Mchezaji wa safu ya ulinzi wa kikosi cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 cha Leicester na Ufaransa Wesley Fofana, 20, anazivutia klabu za Manchester United na Newcastle. (But! Football Club via Sport Witness) mshamuliaji wa Mfaransa Alexandre Lacazette.

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta atakataa ofa yoyote ya kumuuza mshamuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette, 30, mwezi Januar, na badala yake atamruhusu kuondoka kwa uhuru wakati mkataba wake utakapoisha katika msimu ujao. (Sun)

Kipaumbele cha Rudiger ni kubakia Chelsea, lakini mchuano wa kutaka saini yake 'uko wazi'. (Fabrizio Romano) Ousmane Dembele

Manchester City, Tottenham, Liverpool na Newcastle zinamtaka winga Mfaransa Ousmane Dembele, 24, ambaye ana uwezekano wa kuondoka Barcelona msimu ujao. (90Min)

Kiungo wa kati wa England Harry Winks, 25, ameleta mashaka juu ya hali yake ya baadaye katika Tottenham baada ya kukiri kwamba amekuwa aking'ang'ana kurejea katika hali yake bora ya zamani ya kimchezo kama sehemu ya mchezaji wa chini ya Nuno Espirito Santo. (Times - subscription required)

Nahodha wa Newcastle na mlinzi Muingereza Jamaal Lascelles, 27, anasema wachezaji lazima wawajibike kwa kufukuzwa kazi kwa Steve Bruce. (Mail)

Manchester City wanajiandaa kujiunga na Barcelona katika mbio za kusaini mkataba na winga Mbrazili mwenye umri wa miaka 21, Antony kutoka klabu ya Ajax. (El Nacional - in Spanish) Mserbia Filip Djuricic

West Ham na Southampton wanataka kusaini mkataba na mshambuliaji wa kati wa Sassuolo Mserbia Filip Djuricic, 29, ambaye alicheza nusu ya pili ya msimu wa 2014-15 kwa mkopo katika the Saints. (Calciomercato - in Italian)

Everton wanamtaka kiungo wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28, mwezi Januari. (Football Insider)

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer anasema klabu hiyo haijapokea ofa kutoka Everton kwa ajili ya kiungo wake wa Uholanzi Van de Beek, licha ya uwepo wa tetesi nyingi. (RTL7, via Manchester Evening News)

Chanzo: BBC Sports