Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Usajili Ulaya leo Juni 6, 2024

Nacho Fenandez.jpeg Tetesi za Usajili Ulaya leo Juni 6, 2024

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki na nahodha wa Real Madrid, Nacho 34, anatarajiwa kukutana na wawakilishi wa timu hiyo kabla ya wiki hii kumalizika kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye viunga hivyo kwa muda mrefu zaidi. Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na kuna uwezekano akasaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi.

Manchester United imepanga kufanya mazungumzo na wawakilishi wa winga wao, Jadon Sancho dirisha lijalo la majira ya kiangazi kabla ya kuamua juu ya hatma yake. Sancho aliyekuwa akicheza kwa mkopo wa nusu msimu Borussia Dortmund anadaiwa kuwa hana mpango wakuendelea kusalia Man United kwa msimu ujao na badala yake anataka kusaini mkataba wa kudumu na Dortmund.

Kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz, 21, amesisitiza bado hajafikia uamuzi wa hatma yake na kwa sasa anapambana kwa ajili ya kujiweka sawa kucheza michuano ya Euro. Wirtz ni mmoja kati ya mastaa walioonyesha kiwango bora katika kikosi cha kwanza cha Leverkusen katika msimu uliopita ambapo aliisaidia kuchukua ubingwa wa Bundesliga.

Straika wa Manchester City na Argentina Julian Alvarez, 24, ameingia kwenye rada za Atletico Madrid ambayo inafikiria kumnunua mazima au hata kwa mkopo. Alvarez mwenye umri wa miaka 24 amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Man City, hivyo amevutiwa na ofa ya Atletico na kwa mujibu wa ripoti mbalimbali ni hataki kupoteza nafasi hiyo.

Kipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga anatarajia kufanya kikao na kocha mpya wa Chelsea Enzo Maresca kujadili hatma yake msimu ujao. Kepa ambaye msimu uliomalizika alikuwa akicheza kwa mkopo Real Madrid, anahitaji kurudi London kupambania namba kikosi cha kwanza baada ya Madrid kuweka wazi hawana mpango wa kumsainisha mkataba wa kudumu badala yake wanataka kumsainisha mkataba wa msimu mmoja.

Napoli imeiambia Arsenal kama itakuwa tayari kumruhusu straika wao Victor Osimhen aende kujiunga na miamba hiyo ya Emirates kama tu itaweka ubaoni wachezaji wawili kwenye dili hilo. Osimhen anahusishwa na mpango wa kuachana na Napoli kwenye dirisha hili na Arsenal wanatajwa kuhitaji sana huduma yake.

Atalanta ipo Tayari kumuuza staa wao Teun Koopmeiners dirisha hili kwenda Juventus iliyowasilisha ofa inayofikia Euro 40 milioni. Teun ambaye amekuwa kwenye rada za Liverpool kwa muda mrefu, anahitajika na vigogo kutokana na kuwango bora alichoonyesha msimu uliomalizika akiipa Atalanta ubingwa wa Europa League.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live