Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi, Januari 26, 2023

Hakim Ziyech.jpeg Hakim Ziyech

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chelsea wako tayari kuachana na nia yao ya kumnunua winga wa Everton na England chini ya umri wa miaka 21 Anthony Gordon, 21, huku Newcastle pia ikikataa kujiingiza katika vita vya bei ya kumnunua kinda huyo. (Echo)

Gordon hajawasilisha ombi la kutaka uhamisho huko Toffees licha ya kukosa mazoezi katika siku mbili zilizopita. (Sky Sports)

Newcastle wanamfuatilia mshambuliaji wa Chelsea, Hakim Ziyech, 29, kama mbadala wa Gordon kwani hawako tayari kulipa dau la £60m wanalotaka Everton. (Telegraph)

Everton pia wanavutiwa na fowadi huyo wa Morocco na wanaweza kumnasa ikiwa Gordon ataondoka. (Sky Sports)

Chelsea wako tayari kushindana na Liverpool katika mbio za kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ureno wa Wolves Matheus Nunes, 24. (Telegraph).

Mazungumzo ya Everton na Muargentina Marcelo Bielsa kuhusu kuwa meneja wao mpya yamegonga mwamba huku kocha wa zamani wa Southampton Ralph Hasenhuttl akiwa chaguo jingine. (Idependent)

Tottenham wanakaribia kumnunua beki wa pembeni wa Uhispania Pedro Porro, 23, anayechezea Sporting. (Guardian)

Everton wanamfuatilia mshambuliaji wa zamani wa Stoke na West Ham Marko Arnautovic, 33, ambaye anachezea Bologna. (Telegraph)

AC Milan ni moja ya klabu zinazomfuatilia beki wa pembeni wa Manchester City na Ureno Joao Cancelo, 28. (Sun)

Nottingham Forest inafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Inter Milan Muitaliano Roberto Gagliardini, 28. (Calciomercato)

Beki wa pembeni wa Brighton Tariq Lamptey, 22, anaweza kuondoka mwezi huu na Lyon miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa nae. (Fabrizio Romano)

Sporting wamewasiliana na Seagulls kuhusu kumnasa kwa mkopo wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana. (Athletic)

Barcelona wanaweza kumuuza mshambuliaji wa Hispania Ferran Torres katika majira ya joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alijiunga na timu hiyo akitokea Manchester City. (Sport)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live