Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Ulaya 31.10.2021: Kroos, Ramsey, Ten Hag, Jovic, Van de Beek, Barnes

 121281758 8175647b D52e 44a7 A128 E074e5133a1c Toni Kroos

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: BBC Sports

Newcastle inamtaka kiungo wa Real Madrid na Ujerumani Toni Kroos, 31. (El Nacional - in Spanish)

Newcastle pia hawajali kuhusu mshahara anaotaka Aaron Ramsey wanaochataka ni kumsajili kiungo huyo mkongwe wa Wales mwenye miaka 30 kutoka Juventus mwezi Januari. (Tuttosport, via Mirror)

Newcastle inamtaka meneja wa Ajax Erik ten Hag kuwa meneja wake mpya lakini wanakabiliwa na ugumu wa kumshawishi kuachana na waholanzi hao. (Mirror) lovic

Liverpool wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na Serbia Luka Jovic, 23. (Fichajes - in Spanish)

Liverpool itamruhusukipa wake Mjerumani Loris Karius, 28, kuondoka bure mwezi Januari- hajaichezea klabu hiyo tangu mwaka 2018. (Mirror)

Tottenham inakabiliwa na upinzani kutoka kwa Bayern Munich katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Nantes Randal Kolo Muani mwishoni mwa msimu. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka, 22, anamaliza mkataba wake katika majira yajayo ya joto. (Foot Mercato - in French)

Wachezaji wenzie na Donny van de Beek, 24 pale Manchester United wanamuhimiza, muholanzi huyo kubadili wakala wa kumsaidia kuondoka Old Trafford. Mazungumzo yameendelea na vilabu vya Everton na Wolves kuhusu uhamisho wa mkopo. (Mail)

Liverpool inamtaka winga wa Leicester na England Harvey Barnes, 23. (Fichajes - in Spanish)

Tottenham imeungana na Leeds katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Espanyol, mhispania Raul de Tomas, 27. (Sport Witness, via TEAMtalk)

Crystal Palace itakatisha mkataba wa mkopo wa mshambuliaji Jean-Philippe Mateta mwezi Januari. Mfaransa huyo mwenye miaka 24 yuko kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu akitokea Mainz lakini hayuko katika mipango ya meneja wa Palace, Patrick Vieira. (Sun)

Antonio Conte hataki kuchukua timu katikati ya msimu. Meneja huyo wa zamani wa Chelsea na Inter Milan amekuwa akihusishwa na na vilabu vya Manchester United na Newcastle United. (Todofichajes - in Spanish)

Derby inataka kumuuza kipa wake Mscotland David Marshall, 36, katika dirisha la mwezi Januari. (Sun)

Chanzo: BBC Sports