Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Ulaya 30.10.2021: Pogba, Rodgers, Salah, Ronaldo, Hazard, Xavi, Martinez, Saliba

Poga Paul Pp Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: BBC Sports

Manchester United hawatamuuza Paul Pogba na wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya kiungo huyo wa kati wa Kifaransa kuondoka mwishoni mwa msimu kwa uhamisho huru mkataba wake utakapokwisha. (Telegraph)

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers bado ni mbadala muhimu wa Ole Gunnar Solskjaer katika nafasi ya Mkufunzi wa Manchester United. (ESPN)

Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano, 36, anataka bado kuichezea timu ya taifa ya Ureno katika michuano ya kombe la dunia la mwaka 2026. (Sun)

Liverpool wanamtaka mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah,29, kukubali mkataba mpya kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili mwezi Januari. (Football Insider)

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti atamruhusu mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 30, kuondoka kwenye klabu hiyo iwapo atapenda kufanya hivyo. (Marca)

Kocha wa Machester City Pep Guardiola anaamini mkongwe wa Barcelona Xavi yuko tayari kuchukua mikoba ya klabu hiyo ya Uhispania, akisema kuwa mchezaji mwenzake wa zamani ana uzoefu wa uongozi zaidi kuliko yeye alipochukua jukumu hilo. (Goal)

Xavi atajaribu kumuweka winga wa Kifaransa na Bayern Munich Kingsley Coman, 25 kuwa mmoja wa wachezaji wa kwanza atakaowasajili ikiwa atakuwa kocha wa Barcelona. (Sport)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta- mchezaji wa zamani wa timu ya vijana ya Barcelona-amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha nafasi ya ukufunzi iliyoachwa wazi Barcelona. (Sky Sports)

Mlinda mlango wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez,29, anaongoza kwenye orodha ya Tottenham ikiwa Mfaransa Hugo Lloris ataondoka msimu ujao wa majira ya joto. (Independent)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anasema mlinzi wa Ufaransa William Saliba,20 anaweza kuwania nafasi kwenye kikosi cha washika bunduki hao atakaporejea msimu ujao kutoka kwenye klabua ya Marseille alikokuwa akicheza kwa mkopo. (Goal)

Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers amemtaja mchezaji wa Kibelgiji Youri Tielemans kuwa '' mmoja wa viungo wa kati wazuri zaidi Ulaya'' huku Manchester United, Liverpool na Bayern Munich zikihusishwa na mchezaji huyo, mwenye miaka 24. (Mirror)

Mlinzi wa Napoli, Msenegali Kalidou Koulibaly, 30, amesema ataondoka kwenye klabu hiyo kuelekea Manchester City, Real Madrid au Barcelona. (Sport Witness)

Mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, mwenye miaka 24 ambaye alikuwa akitakiwa na Manchester City- anajiandaa kusaini mkataba mpya na Inter Milan. (Manchester Evening News)

Kocha wa Crystal Palace Patrick Vieira ilikuwa ''furaha'' kufanya kazi na kiungo wa kati wa Kiingereza Conor Gallagher, aliyecheza kwa mkopo kutoka Chelsea, lakini alisema ilikuwa mapema kujadili kuhusu uhamisho wa kudumu. (Independent) Patrick Vieira

Kocha wa muda wa Newcastle United Graeme Jones amesema ana uhakika wa kuwa angalau meneja msaidizi wa klabu hiyo siku zijazo - bila kujali ni nani atateuliwa kuwa kocha mkuu.(Chronicle)

Arsenal wanamtolea macho winga wa Club Bruges, Mholanzi Noa Lang,22, na wamepata nguvu zaidi wakati Borussia Monchenglabach kusitisha nia ya kumnasa mchezaji huyo. (Football.London)

Chanzo: BBC Sports