Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Ulaya 10.10.2021: Koulibaly, Tarkowski, Icardi, Pogba, Dembele,

 121010922 21c3f780 Bd3f 4e49 B6ee 958cd7719ef3 Mlinzi wa kati wa Napoli Kalidou Koulibaly

Sun, 10 Oct 2021 Chanzo: BBC Sports

Newcastle United inapanga uhamisho wa mlinzi wa kati wa Napoli Kalidou Koulibaly,30. (Football Insider).

Mlinzi wa Burnley James Tarkiwski,28 anaweza kuwa mmoja wa wachezaji wa kwanza kusajiliwa na Newcastle, huku klabu hiyo ikiwa imemjadili mchezaji wa England Jesse Lingard, huku kiungo mshambuliaji huyo, 28, akitarajiwa kumaliza mkataba wake na klabu ya Manchester United msimu ujao wa joto. (Sunday Telegraph)

Newcastle pia inavutiwa na mshambuliaji wa Paris St-Germain na raia wa Argentina, Mauri Icardi, ingawa Tottenham na Juventus pia zinamtolea macho mchezaji huyo mwenye miaka 28. (Calciomercato,via Mail on Sunday)

Wamiliki wapya wa Newcastle wanajiandaaa kumfukuza kocha Steve Bruce juma lijalo. (Sunday Mirror)

Juventus inaweza kuwa na nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa, Paul Pogba, ambaye mkataba wake na Manchester United uko mbioni kumalizika, ikiwa wataweza kuwauza takribani wachezaji wawili. (La Gazzetta dello Sport)

Liverpool wanapanga kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa, Ousmane Dembele kwa uhamisho huru wakati mkataba wa mchezaji huyo na Barcelona ukikaribia kuisha kipindi cha majira ya joto. (Teamtalk)

Leeds United wanaamini kuwa kiungo wa kati wa England Kalvin Phillips ataongeza mkataba wake na klabu hiyo kabla ya mwishoni mwa mwaka, wakati mazungumzo yakiwa kwenye hatua za mwishoni . (Football Insider)

Manchester United wanajiandaa kuanza mazungumzo na mlinzi wa kati wa England Harry Maguire kuboresha masharti ya mkataba wa mchezaji huyo mwenye miaka 28. (Sunday Mirror)

Inter Milan wanamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette,30, pia mshambuliaji wa Real Madrid Mserbia Luka Jovic, 23, kama machaguo ya mwezi Januuari. (La Gazzetta dello Sport)

Sevilla wanapima uhamisho wa mshambuliaji wa Blackburn Rovers na Chile mwenye umri wa miaka 22 Ben Brereton, huku mshambuliaji wa kilabu cha Uhispania Yorsef En-Nesyri, 24, akihusishwa na kuhamia Arsenal au Tottenham. (Teamtalk)

Chanzo: BBC Sports