Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Ulaya 08.11.2021: Sterling, De Jong, Vlahovic, Lampard, Zidane, Gerrard, Traore, Ramos

Pep Sreling Meneja wa City, Pep Guardiola akiwa na Sterling

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: BBC Sports

Manchester City huenda ikaiomba Barcelona kuwapatia kiungo wakati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 24, ikiwa klabu hiyo ya Uhispania inataka kumsajili winga wa England Raheem Sterling, 26. (El Naciona)

Mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic huenda akakataa kuhamia Arsenal mwezi Januari kwa sababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia wa miaka 21- anasubiri ofa zingine. (Football Italia)

Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Frank Lampard ameanza mazungumzi na Norwich City kuhusu kuwa maneja mpya wa klabu hiyo ya Carrow Road. (Football Insider)

"Haiwezekani" kwa kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuchukua nafasi ya meneja wa Manchester United ikiwa Old Trafford itamfukuza Ole Gunnar Solskjaer. (AS - in Spanish)

Orodha ya Aston Villa ya wanaoweza kuchukua nafasi ya Dean Smith aliyetimuliwa ni pamoja na kocha wa Rangers Steven Gerrard, meneja wa Southampton Ralph Hasenhutl na kocha mkuu wa Denmark Kasper Hjulmand. (Telegraph - subscription required)

Mkufunzi wa Wolves Bruno Lage anasema hali ya mkataba wa Adama Traore katika klabu hiyo haitamzuia kumchagua winga huyo wa Uhispania kwa upande wa Molineux. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amesalia na miezi 18 katika mkataba wake wa sasa. (Mail) Wolves ndio klabu inayovutiwa zaidi na kiungo wa kati wa Lille na Ureno Renato Sanches na wanaweza kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 mwezi Januari. (Fichajes.net)

Beki wa Uhispania Sergio Ramos hana mpango wa kuondoka Paris St-Germain, kulingana na kaka na wakala wa Rene mwenye umri wa miaka 35. Beki huyo wa kati alijiunga na klabu hiyo ya Ufaransa kwa uhamisho wa bure msimu wa joto baada ya kuondoka Real Madrid lakini bado hajaichezea kwa sababu ya jeraha. (El Mundo, via Goal)

Mkataba wa kiungo wa Inter Milan Marcelo Brozovic unakamilika msimu ujao wa joto na, akizungumzia kuhusu kuongezwa kwa kandarasi, mkurugenzi wa klabuu hiyo ya Series A, Beppe Marotta, anasema "wachezaji wanajali Inter na wanataka kuendelea hapa". (DAZN, via Football Italia)

Chanzo: BBC Sports