Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Ulaya 04.10.2021:Aurier, Ranieri, Gonzalez, Werner, Toure, Sanchez

Tetesi Serge Aurier

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: BBC Sports

Mlinzi wa Ivory coast Serge Aurier, 28, ambaye sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Tottenham Hotspurs, anajiandaa kujiunga na Villarreal ya Uhispania.(L'Equipe - in French)

Claudio Ranieri amekubali kuwa kocha mkuu mpya wa Watford baada ya kuondoka kwa Xisco Munoz siku ya Jumapili, huku Muitaliano huyo, 69 akitarajiwa kuweka saini Jumatatu. (Sky Sports)

Manchester City wanamfuatilia kiungo wa kati wa Uhispania Nico Gonzalez anayekipiga Barcelona, ambaye hajapewa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza (Fichajes - in Spanish)

Mlinzi kinda wa Kijerumani anayecheza katika klabu ya Borussia Monchengladbach Luca Netz anadai alikataa uhamisho aliosema ''hauna maana'' kwenda Manchester City miaka mitatu iliyopita, mchezaji huyo mwenye miaka 18 anasema atawakatalia kwa mara nyingine tena. (Sun)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Alexis Sanchez hajui mustakabali wake Inter Milan baada ya mchezaji huyo mwenye miaka 32-kuchapisha kisha kufuta ujumbe uliokuwa ukikosoa kitendo cha kukosa muda wa kucheza uwanjani. (Mirror)

Atletico Madrid nayo imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnasa mshambuliaji Timo Werner, 25 anayekipiga Chelsea. (Transfer Market Web)

Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure, 38, ametoa ofa kwa Barcelona wakati huu wakiwa katika changamoto, lakini haijulikani kama raia huyo wa Ivory coast anataka kucheza au kufundisha. (Sun)

Mike Ashley anajua njia pekee ya kumbadili kocha mkuu wa Newcastle ni kulipa karibu kila kandarasi ya Steve Bruce ambayo alikubali mnamo Julai 2019.(Chronicle Live)

Mshambuliaji wa Kiholanzi anayecheza Bayern Munich Joshua Zirkzee, 20, anasema alikataa nafasi ya kujiunga na Everton mwaka 2017. (Het Nieuwsblad via Liverpool Echo)

Chanzo: BBC Sports