Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Januari 10

Ndombeleee Kiungo wa Tottenham Hotspurs, Tanguay Ndombele

Mon, 10 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Ghali ndani ya Kikosi cha Tottenham, Tanguy Ndombele, ana matumaini ya kuondoka Tottenham Hotspur mwezi huu. (The Athletic - subscription required)

Winga wa Uholanzi Steven Bergwijn anaonekana kukaribia kuondoka Spurs, huku Ajax ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. . (Fabrizio Romano on Twitter)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Mfaransa Kylian Mbappe, 23, bado anaweza kukataa kuhamia Real Madrid na kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Le Parisien - in French)

Mshambulizi wa Bayer Leverkusen na Jamhuri ya Czech Patrik Schick, 25, anasema ana furaha katika klabu hiyo ya Bundesliga licha ya uvumi kuhusu kuhama mwezi Januari. (Bild - in German)

Aston Villa wako katika mazungumzo ya juu zaidi kumnunua Lucas Digne kutoka Everton, huku beki huyo wa kushoto wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 akiaminika kupendelea kuhamia kikosi cha Steven Gerrard. (Sky Sports)

Newcastle United wamewasiliana na Burnley kumnunua mshambuliaji wa New Zealand Chris Wood, 30. (Telegraph - subscription required)

The Magpies pia wamemuongeza mshambuliaji wa RB Salzburg ya Uswizi Noah Okafor, 21 kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kusajiliwa mwezi huu. (Teamtalk)

Kipa wa zamani wa Newcastle Shay Given amemshauri mwenzake Caoimhin Kelleher, 23, kuondoka Liverpool katika dirisha la uhamisho la mwezi huu ili kipa huyo wa Jamhuri ya Ireland apate muda zaidi wa kucheza. (Premier Sport via Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Crystal Palace Jean-Philippe Mateta anakaribia kuondoka katika klabu hiyo mwezi huu huku fowadi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Mainz, akitarajiwa kuhamia kwa mkopo St Etienne inayoshiriki Ligue 1. (Standard)

Beki wa Arsenal, Sead Kolasinac amefanya mazungumzo na Marseille kuhusu uhamisho wa bila malipo msimu wa joto, huku beki huyo wa kushoto wa Bosnia, 28, akiwa hana nafasi kwenye Uwanja wa Emirates. (L'Equipe via Sun)

Kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel amependekeza kiungo wa kati wa Uingereza Ross Barkley, 28, anaweza kuruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo mwezi huu. (90 Min)

Kiungo wa kati wa Manchester City Tommy Doyle amemaliza muda wake wa kuitumikia Hamburg, huku Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 20 akitarajiwa kuhama kwa muda mfupi nje ya Uwanja wa Etihad mwezi huu. (Manchester Evening News)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live