Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Januari 1

Coutinho 2021 22 Season Philipe Coutinho

Sat, 1 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tottenham wanataka kusaini mkataba na mchezaji nyota wa Barcelona na Brazil mwanye umri wa miaka 29, Philippe Coutinho kwa uhamisho huru.Barcelona wanataka Pauni Milioni 17 huku Arsenal na Everton wakionesha nia.

Manchester United wako tayari kulipa pauni milioni 16.8 zinazohitajika kwa ajili ya kipengele cha mkataba cha kitakachowawezesha kusaini mkataba na mshambuliaji wa River Plate Muargentina Julian Alvarez mwezi Januari , huku wakiwa mbele ya having Bayern Munich, Barcelona, Real Madrid na Inter Milan katika mbio za kusaini mkataba na kijana huyo mwamye umri wa miaka 21. (Sport - in Spanish)

Newcastle wanakaribia kufikia mkataba kwa ajili ya beki wa kulia wa Atletico Madrid Muingereza Kieran Trippier, 31, huku kukiwa na vipengele vinavyohusu kushuka kwa daraja la Primia Ligi vikiwa miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa. (Athletic - subscription required)

Chelsea watalazimika kutoa ofa ya mlinzi wa kati Mjerumani Antonio Rudiger, 28, ya malipo ya juu zaidi kwa wiki kuliko mchezaji yeyote yule wa the Blues ili kumshawishi aongeze zaidi mkataba wake ambao unaisha mwishoni mwa msimu . (Football Insider)

Rudiger anataka kusaini marupurupu ya zaidi ya pauni milioni 16 kwenye mkataba wake na Chelsea na asaini mkataba na Real Madrid kama wakala huru katika msimu huu . (ABC - in Spanish)

Tottenham bado wanaendelea kumtazama mshambuliaji wa Wolves na Uhispania mwenye umri wa miaka 25 Adama Traore. (Fabrizio Romano via This is Futbol)

Manchester City wanajiandaa kumruhusu winga mwenye umri wa miaka 19 anayetazamiwa kufanya vyema siku zijazo Mholanzi Jayden Braaf kuondoka kwneye klabu hiyo Januari huku klabu kadhaa zikimtaka kwa mkataba wa bei nafuu huku akikaribia kumaliza mkataba wake. (Manchester Evening News)

Sunderland wanakaribia kukamilisha mkataba na winga wa Manchester City mwenye umri wa miaka 24 Patrick Roberts. Muingereza huyo kwa sasa anacheza kwa mkataba wa mkopo katika klabu ya Ufaransa ya Troyes. (Football Insider)

Chelsea wanakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Monaco Mfaransa Aurelien Tchouameni, 21, ambaye anaweza kuwa chaguo nafuu kuliko nyota wa West Ham na England Declan Rice, 22. (Daily Telegraph's Matt Law on the London is Blue podcast, via Chelsea Chronicle)

Leeds wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Giovanni Simeone, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Verona kutoka Cagliari, majira ya joto. (L'Arena, via Sport Witness)

Barcelona wamemfanya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Alvaro Morata, 29, ambaye kwa sasa yuko Juventus kwa mkopo kutoka Atletico Madrid, kuwa lengo la kuu la Januari. (AS - in Spanish)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live