Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Februari 28

La Pulga Messi.jfif Lionel Messi

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inter Miami itapambana kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kama nyota huyo mwenye miaka 34 ataamua kuondoka Paris St-Germain, anasema mmiliki mwenza wa klabu hiyo ya ligi kuu ya Marekani. (Goal)

Mkataba wa mshambuliaji wa Poland, Robert Lewandowski pale Bayern Munich unamalizika mwaka 2023, wakati mkongwe huyo mwenye miaka 33 akitaka mkataba mpya kusalia katika klabu hiyo ya Ujerumani, hakuna mazungumzo yaliyofanyika mpaka sasa. (Fabrizio Romano).

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway, Erling Braut Haaland hajakubali kujiunga na Real Madrid katika dirisha lijalo la majira ya joto, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake na mshambuliaji wa zamani wa Middlesbrough Jan Aage Fjortoft,21. (Mundo Deportivo)

Barcelona wanakaribia kumsajili kiungo wa Ivory Coast Franck Kessie kwa uhamisho huru wakati mkataba wa nyota huyo wa AC Milan mwenye umri wa miaka 25 utakapomalizika. (Sport - in Spanish)

Newcastle United ilishindwa kumsajili mlinzi wa Uholanzi, Sven Botman mwezi Januari, na kinda huyo mwenye miaka 22 ambaye anahusishwa pia na Tottenham, anatarajia kujiunga na AC Milan katika majira yajayo ya joto. (Todofichajes)

Andreas Christensen ameelezea suala lake ndani ya Chelsea ni "gumu", huku mkataba wa mlinzi huyo wa Denmark mwenye miaka 25 ukielekea ukingoni mwisho mwa msimu. (90 Min)

Mlinzi wa Sporting Lisbon mreno Goncalo Inacio amekubali kusaini mkataba mpya kusalia klabuni hapo. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa akiwaniwa na Newcastle United katika dirisha la mwezi Januari. (Fabrizio Romano)

Klabu za Real Sociedad na Atalanta zinamuwania kwa mkopo mlinzi wa kushoto mgiriki Dimitris Giannoulis kutoka Norwich City. (Norfolk Live)

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Roy Keane ameiambia klabu hiyo kumpa mikoba ya ukocha, kocha wa sasa wa Atletico Madrid Muargentina Diego Simeone. (Goal)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live