Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Februari 26

Why NGolo Kante Didnt Play Against Norwich Kiungo wa Chelsea, Ngolo Kante

Sat, 26 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi zinasema, Paris St-Germain huenda wakamnunua kiungo wa kati wa Chelsea Mfaransa N’Golo Kante,30, msimu wa joto.

Kocha wa PSG Muargentina Mauricio Pochettino, 49, amepuuza wito wa Manchester United kumtaka ajiunge nao Old Trafford anaposubiri kuchukua usukani Real Madrid.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 28, huenda akaomba kuondoka Tottenham kwa mara nyingine tena ikiwa Antonio Conte ataacha kazi kama kocha wa Spurs.

Kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 31, huenda akaondoka PSG baada ya kuwaepo kwa msimu mmoja pekee, akihusishwa na klabu za Atletico Madrid, West Ham, Newcastle United and Aston Villa.

Arsenal wameungana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak lakini wanataka Real Sociedad kupunguza bei ya ya kiungo huyo wa miaka 22- kwa kuzingatia kifungu cha kumuachilia ili kufikia mkataba.

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 28, anasemekana yuko radhi kuhamia Paris St-Germain, kulingana na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea striker na Mfaransa mwenzake Nicolas Anelka.

Tetesi zinasema, Beki wa RB Leipzig Mhispania Angelino huenda akaondoka klabu hiyo ya Ujerumani msimu wa joto, huku Arsenal, Tottenham na Barcelona zikihusishwa na kiungo huyo wa miaka 25.

West Ham, Leicester City na Everton zimehusishwa na tetesi za kutaka kumnunua kiungo wa Bristol City Alex Scott, huku Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 18 pia akivutia kutoka nje ya nchi.

Tetesi zinasema, Aston Villa wanasemekana kuwa tayari kupokea ofa ya kumnunua mlinzi wa zamani wa England chini ya miaka 21 Ezri Konsa, 24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live