Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Disemba 9

Ramsey Aron Ramsey

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: BBC Sports

Kiungo wa kati wa Juventus na Wales Aaron Ramsey huenda akajiunga na klabu ya Everton mwezi Januari , huku klabu hiyo ya serie A ikifurahia kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye ameichezea klabu hiyo mara tano pekee msimu huu. (Calciomercato - in Italian)

Hilo ni pigo kwa Newcastle , ambao walikuwa na mataumaini kwamba Ramsey atakuwa mchezaji wake wa kwanza kusajiliwa chini usimamizi mpya wa klabu hiyo. (Star)

Wachezaji kadhaa wa Chelsea hawafurahii kwanini klabu hiyo haijamuongezea kandarasi Cesar Azpilicueta huku Atletico Madrid ikiwa na hamu na beki huyo wa Uhispania, 32. (Eurosport)

Beki wa kushoto wa Real Madrid Marcelo, 33,anatarajiwa kukamilisha kandarasi yake baada ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka 15 wakati itakapokamilika mwaka ujao na kujiunga na klabu ya Fluminense nchini Brazil.(Mirror)

Klabu ya PSG iko tayari kuchukua maombi ya mkopo kwa aliyekuwa kiungo wa kati wa Liverpool Georginio Wijnaldum katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 raia wa Uholanzi yuko tayari kurudi katika ligi ya Premia na tayari Arsenal wanamlenga. (Sky Sports)

Newcastle, ambayo pia ni klabu ya zamani ya Wijnaldum pia huenda ikawasilisha ombi la kumsajili raia huyo wa Uholanzi katika dirisha la uamisho la mwezi Januari. (Marca)

Newcastle Inawalenga wachezaji watano katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari , ambao ni pamoja na kiungo wa kati wa Misri Mohammed Elneny 29.. (Mirror)

Mkufunzi wa Everton Rafael Benitez aliwamcha nje Lucas Digne, 28, katika ushindi dhidi ya Arsenal kufuatia mgogoro na sasa beki huyo wa kushoto wa ufaransa huenda akauzwa mnamo mwezi Januari.. (The Athletic - subscription required)

Mkufunzi mpya wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick amesema anatumai atashirikiana na mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani katika kipindi kilichosalia cha msimu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 amehusishwa na uvumi wa kuondoka Old Trafford. (Manchester United)

Mkufunzi wa klabu ya West Ham David Moyes atapatia kipaumbele usajili wa beki mwezi Januari baada ya wachezaji Kurt Zouma na Angelo Ogbonna kupatikana na majeraha.(Mail)

Arsenal inatumai kuweka makubaliano na mchezaji wa Juventus na Uswidi mwenye umri wa miaka 21 Dejan Kulusevski. (La Repubblica, via Sun)

Besiktas inataka kufuta kandarasi ya mchezaji aliye katika klabu hiyo kwa mkopo wa muda mrefu Miralem Pjanic na kumrudisha raia huyo wa Bosnia na Herzegovina, 31, Barcelona.(Zurnal - in Bosnian)

Chanzo: BBC Sports