Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Disemba 29

Mbappeeee Kylian Mbappe

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe anasema hatahamia Real Madrid mwezi Januari na atasalia Paris St-Germain hadi angalau mwisho wa msimu. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 na timu hiyo ya Ligue 1 unamalizika msimu wa joto(CNN)

Winga wa Leeds United Raphinha amekuwa akihusishwa na Liverpool na Bayern Munich, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 hatashinikiza kuhama mwezi Januari. (Mirror)

Barcelona haijakata tamaa katika kujaribu kumsajili mlinzi wa Uhispania Cesar Azpilicueta, 32, na beki wa kati wa Denmark Andreas Christensen, 25, kutoka Chelsea. (Sport - in Spanish)

Everton wamejadili uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 na mchezaji wa zamani Ross Barkley kwa mkopo kutoka Chelsea wakati wa dirisha la uhamisho la Januari. (Telegraph - subscription required)

Chelsea wanafikiria kujaribu kumsajili beki wa kushoto wa Everton Lucas Digne, 28, wa Ufaransa, huku timu hiyo ya Stamford Bridge ikamkosa beki wa Uingereza Ben Chilwell, 25, kwa kipindi kirefu kwa sababu ya jeraha la goti. (90 Min)

Mshambulizi wa Jamhuri ya Czech Patrik Schick, 25, analengwa na vilabu kadhaa vya Premier League - akiwa ametazamwa na Arsenal, Everton, Manchester City, Tottenham na West Ham katika miezi ya hivi karibuni - lakini Bayer Leverkusen hawana haraka ya kumuuza mchezaji huyo ambaye yuko chini ya mkataba hadi 2025. (90 Min)

Newcastle United wanapanga kumnunua beki wa kati wa Ufaransa Samuel Umtiti, huku Barcelona wakitamani kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Marca)

Newcastle pia wana nia ya kumleta mshambuliaji wa Brazil Gabriel Barbosa mwezi Januari, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 angependelea kusalia na Flamengo. (Mirror)

Mshambuliaji wa Italia Lorenzo Insigne, ambaye kandarasi yake na Napoli inakamilika msimu wa joto, anashawishiwa na ofa kutoka kwa Toronto FC, na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Soka inashinikiza kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 mwezi Januari. (Sky Sport Italia, via Football Italia)

Juventus wanataka kubadilisha masharti ya kuongeza mkataba yaliyokubaliwa na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 28, ambaye atakuwa huru kuondoka katika klabu hiyo mkataba wake wa sasa utakapokamilika msimu wa joto. (La Gazzetta dello Sport, via Football Italia)

Queens Park Rangers wako mbele ya Nottingham Forest katika kujaribu kumsajili beki Mwingereza Steve Cook mwenye umri wa miaka 30 kutoka Bournemouth. (Mail)

Middlesbrough wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Aaron Connolly, 21, kwa mkopo kutoka Brighton. (Mail)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live