Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Disemba 28

Kessie Kessie Frank Kessie

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tottenham wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie, ambaye mkataba wake na AC Milan unakamilika msimu wa joto. Arsenal na Manchester United pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 lakini Spurs tayari wamefanya mazungumzo na kambi ya Kessie. (Express)

Mkufunzi wa Newcastle United Eddie Howe hataki kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham Muingereza Dele Alli mwenye umri wa miaka 25 kwa vile anataka kuimarisha sehemu nyingine za timu yake mwezi Januari. (Football Insider)

Chelsea wako tayari kushindana na Liverpool kujaribu kumsajili winga wa Brazil Raphinha, 25, kutoka Leeds United msimu wa joto. (Sport Italia, via Express)

Real Madrid wanavutiwa na beki wa kulia wa Chelsea na England Reece James, 22, na wanaweza kujaribu kuwajaribu The Blues kwa kumpa winga wa Ubelgiji Eden Hazard kama sehemu ya mkataba wowote. (El Nacional - in Catalan)

Kipaumbele cha Real Madrid ni kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21, kutoka Borussia Dortmund msimu ujao lakini klabu hiyo ya Uhispania inamtazama mshambuliaji wa Fiorentina mwenye umri wa miaka 21 na Serbia Dusan Vlahovic kama mbadala wake iwapo watamkosa. (El Nacional - in Catalan)

Winga wa Chelsea na Uingereza Callum Hudson-Odoi, 21, analengwa na Napoli, ambayo inanolewa na mkufunzi wa zamani wa Blues Maurizio Sarri. (Tuttosport, via Football Italia)

Barcelona wanataka kumuachilia huru mchezaji wa Brazil Philippe Coutinho na chaguo analopendelea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ni kwenda Arsenal. (Sport - in Spanish)

Klabu ya Ufaransa Lille inataka angalau Euro milioni 30 (Pauni milioni 25) ikiwa watalazimika kumuuza mlinzi wa Uholanzi Sven Botman, 21. (Tuttomercatoweb - in Italian)

Mshambulizi wa Italia Andrea Belotti yuko tayari kuondoka Torino wakati mkataba wake na timu hiyo ya Serie A utakapokamilika msimu wa joto, huku AC Milan, Napoli na Fiorentina zikimwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Calciomercato, via Football Italia)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live