Tetesi zinasema, mshambuliaji Gareth Bale, 32, na kiungo Isco, 29, ndio wachezaji wanaopigiwa upatu kuondoka Real Madrid mwezi Januari, huku kandarasi za wachezaji wote wawili zikimalizika msimu wa joto.
Real Madrid inazidi kuwa na uhakika wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe kutoka Paris St-Germain licha ya klabu yake kugoma kumuachia.
Real Madrid pia wanatarajia mlinzi wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, 28, kujiunga nao bila malipo mwishoni mwa msimu huu. Huku ikiwa imesalia miezi sita pekee katika mkataba wake.
Mshambulizi wa Manchester City Ferran Torres, 21, yuko nchini kwao Uhispania na atafanyiwa vipimo vya afya leo kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Barcelona.
Manchester United inalenga wachezaji wanne wa Ujerumani wanaotarajiwa kuwasajili. Kiungo wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz, 18, mlinzi wa kushoto wa Borussia Monchengladbach mwenye umri wa miaka 18 Luca Netz, kiungo wa kati wa RB Lepizig Eric Martel na beki wa kati wa VfL Bochum Armel Bella-Kotchap, 20.
Newcastle United wanapanga kumsajili kiungo wa Marseille Boubacar Kamara. Mfaransa huyo atakua mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu, huku Manchester United na Chelsea pia zikivutiwa.
Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Uingereza Ainsley Maitland-Niles, 24, yuko tayari kuondoka Arsenal na kujiunga na Roma ya Italia kwa mkopo.
Tetesi zinasema, Mkufunzi wa West Ham David Moyes anamtaka beki wa kati, Lloyd Kelly, 23, kutoka Bournemouth ili kusaidia kukabiliana na matatizo ya safu ya ulinzi ya timu yake.
Tetesi zinasema, Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel amependekeza kiungo wa kati wa Uingereza Conor , 21, atarejea Stamford Bridge baada ya kumalizika kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu ya Crystal Palace.
Nahodha wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza John Terry anatarajiwa kurejea klabuni hapo kusaidia maendeleo ya vijana. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 aliacha nafasi kama msaidizi wa kocha wa wakati huo wa Aston Villa Dean Smith msimu wa joto.