Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Disemba 26

Raphinha Raphinha

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji anayelengwa na Arsenal, Chelsea na Manchester City Dusan Vlahovic huenda akaondoka katika klabu yake katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari kwasababu mshambuliaji huyo wa Fiorentina anataka kulipwa mshahara wa Pauni laki 200,000 kwa wiki. (Star)

Manchester United wanamfuatilia kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen mwenye umri wa miaka 18 Florian Wirtz - anayefahamika kuwa 'Kai Havertz' mtarajiwa kama mchezaji huru. (Express)

Kipa wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez, 29, ni miongoni mwa makipa wanaolengwa na Manchester United ili kumrithi David de Gea, 31. (Star)

Licha ya uvumi kuhusu mipango ya Januari ya klabu ya Newcastle, mkufunzi mkuu Eddie Howe anasema kwamba timu hiyo lazima iwe na uhakika kuhusu fursa walio nayo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.. (Express)

Rafael Benitez ana matumaini kwamba mshambuliaji wa Everton mwenye umri wa miaka 18 Lewis Dobbin atasaini mkataba mpya kubaki Goodison Park. (Liverpool Echo)

Liverpool ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa West Ham Jarrod Bowen , 25 winga wa Leeds na raia wa Brazil Raphinha, 25. (Liverpool Echo)

Baada ya kutumia Pauni milioni 150 katika kipindi cha msimu wa joto, mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta atawekeza zaidi katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Express)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live