Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Disemba 25

Spurs Midfielder Dele Alli  674x420 Kiungo wa Tottenham Hotspurs, Dele Alli

Sat, 25 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Arsenal inamnyatia mshambuliaji wa Sevilla Youssef En-Nesyri kwa lengo la kumsajili dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. Kwa kuwa bei ya Dominic Calvert-Lewin na Dusan Vlahovic iko juu, the Gunners wanapania kumfanya mshambuliaji huyo wa miaka 24- wa Morocco kuwa mmbadala. (Express)

Tottenham wako tayari kumuachilia kwa mkopo kiungo wakati wa Uingereza Dele Alli, 25, mwezi Januari, naye beki wa Ireland Matt Doherty, 29, anaweza kuondoka kwa mkataba wa kudumu. (Evening Standard)

Winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, amekubali mkataba mpya wa miaka mitano na Barcelona, kwa masharti yaliyopunguzwa, na atatia Saini makubaliano hayo wiki ijayo. (Sport)

Kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 26, anayehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United, anataka kurefusha mkataba wake na Leeds United. (Mail)

Roma wanafanya mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Ainsley Maitland-Niles, 24, mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguli. (ESPN)

Mshambuliaji wa Orlando City na Marekani Daryl Dike, 21, anasakwa na klabu kadhaa za Uingereza ikiwemo West Ham, Newcastle, Brighton, Leeds na West Brom. (Team Talk)

Atletico Madrid inatarajia kupokea dao la kumuuza beki wa Uingereza wa miaka 31- Kieran Trippier fkutoka kwa Newcastle United mwezi Januari. (ESPN)

West Ham, Crystal Palace na Brighton ni miongoni mwa klabu zinazomtaka mshambuliaji wa Arsenal Muingereza English Eddie Nketiah, 22. (Mail)

Newcastle United wamesitisha mpango kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 26, kwa sababu itawagharimu pauni milioni sita kumchukua kwa mkopo kwa kipindi cha pili cha msimu. (Football Insider)

Mlinzi wa Ufaransa Clement Lenglet, 26, anataka kusalia Barcelona, licha ya kupoteza nafasi ya kikosi cha kwanza msimu huu. (Marca)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live