Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Disemba 24

Edson Cavani Ed Mshambuliaji wa Man United, Edson Cavani

Fri, 24 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sevilla wamejiunga na Barcelona katika kinyang'anyiro cha usajili wa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34, Manchester United. (Mundo Deportivo - in Spanish)

AC Milan wanamatumaini ya kumsajili winga wa Chelsea na Morocco Hakim Ziyech, 28. (Calciomercato - in Italian)

Liverpool wanapania kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Eduardo Camavinga, 19. (El Nacional - in French)

Newcastle United wamewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 24, ijapokuwa klabu hiyo ya Uhispania inajaribu kurefusha mkataba wake. (Fabrizio Romano)

Tottenham wanatathini uwezekano wa kumnunua beki wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 22. (4-4-2 via Sun)

Kiongo wa kimataifa wa Uingereza na Arsenal wachini ya miaka 21 Eddie Nketiah, 22, anataka kuondoka kwa ajili ya kutaka kucheza katika kikosi cha kwanza licha ya The Gunners kutaka kuongeza mkataba wake utakaokamilika msimu ujao wa joto. (Mail)

Juventus wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Mfaransa Anthony Martial, 26, na mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 32. (Gazzetta dello Sport, usajili unahitajika)

Meneja wa Tottenham Antonio Conte ameamua kusalia na winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 24, katika klabu hiyo licha ya vilabu vya kadhaa kumtaka. (Sky Sports)

Chelsea wana nia ya kumnunua beki wa Barcelona na Marekani Sergino Dest, 21. (El Nacional - via Metro).

Tottenham kwa sasa wanaongoza katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa kati wa AC Milan na Ivory Coast Franck Kessie. Timu hiyo ya kaskazini mwa London italazimika kupambana na Paris St-Germain, ambao pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Klabu hiyo ya Italia pia ina nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Fulham mwenye umri wa miaka 27 kutoka Serbia Aleksandar Mitrovic. (90 Mins)

Ralf Rangnick anajiandaa kuwasiliana na klabu yake ya zamani ya RB Leipzig kumnunua kiungo wa kati wa Mali Amadou Haidara, 23, huku akitafuta mbadala wa Nemanja Matic, 33, raia wa Serbia. (Mirror)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live