Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Disemba 22

Thumb 113473 Default News Size 5.jpeg Joe Gomez

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Real Madrid wanamfuatilia kwa karibu beki wa England na Liverpool Joe Gomez, 24. (Mail)

Manchester United, Barcelona na Real Madrid zote zinafuatilia kwa karibu winga wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman, 25. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Liverpool wanashindania Saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 21 Mnorway Erling Braut Haaland. (Sky Germany)

Mshambuliaji wa kati wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 26, anataka kujiunga na Sevilla kwa mkopo. (Sky Sports)

Manchester United wamewasiliana na River Plate kuhusiana na kusiani mkataba wa pauni milioni 17 kwa ajili ya mshambuliaji Muargentina mwenye umri wa miaka 21, Julian Alvarez. (Ole - in Spanish)

Nahodha wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 32, anataka kubaki katika klabu hiyo licha ya Barcelona kuonyesha nia ya kusaini mkataba na mlinzi huyo Muhispania wakati mkataba wake utakapomalizika msimu huu. (The Athletic - subscription required)

Tottenham Hotspur na Roma wanagombania sahihi ya kiungo wa kati wa Hoffenheim na Ujerumani Florian Grillitsch, 26. (Sky Germany)

Manchester United wana nia ya kusaini mkataba na mchezaji wa Lazio Mserbia Sergei Milinkovic-Savic, 26. (Il Messaggero - in Italian)

Chelsea ilikuwa na dau la pauni milioni 72 kwa ajili ya mlinzi wa Paris St-Germain Marquinhos, 27, ambalo alilikataa msimu huu. (L'Equipe - in French)

Kiungo wa Brazil Marquinhos atasaini mkataba mpya katika PSG hadi mwaka 2026 au 2027. (Fabrizio Romano)

Everton watafanya jaribio la tatu kusaini mkataba na kiungo wa Rangers na Uskochi Nathan Patterson, 20. (Guardian)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live