Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Disemba 21

Anthony Martial 21 Mshambuliaji wa Man United, Anthony Martial

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Newcastle United wako makini kuimarisha safu yao ya mashambulizi katika dirisha dogo la mwezi Januari huku mshambuliaji wa Manchester United Mfaransa Anthony Martial mwenye umri wa miaka 26 na mshambuliaji wa Inter Milan Mbosnia Edin Dzeko, mwenye umri wa miaka 35, wakiwa kwenye orodha yao. (Sun)

Everton imekubali mkataba wa pauni milioni 17, kwa ajili ya Vitaliy Mykolenko, 22, na hivyo kupata njia ya kumuondoa katika the Toffees mlinzi Mfaransa Lucas Digne, 28, huku Newcastle na Leicester zikiwa na nia ya kumchukua. (The Mirror)

Manchester United inakaribia kummleta Old Traffpord kiungo wa kati mwenye thamani ya juu Mfaransa Boubacar Kamara, mwenye umri wa miaka 22, kutoka klabu ya Marseille katika kile kitakachokuwa ni hatua ya kwanza kabisa ya Ralf Rangnick kusaini mkataba na mchezaji kama meneja wa mpito . (FourFourTwo)

Manchester United wamejiunga katika kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na mshambuliaji wa River Plate na Argentina Julian Alvarez, 21. (Ole - via Metro)

Real Madrid wako katika mazungumzo na Antonio Rudiger yenye azma ya kusaini mkataba na mlinzi huyu wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 28, wakati mkataba wake utakapomalizika katika klabu ya Chelsea mwezi Juni mwakani. (Rudy Galetti)

Everton inaweza kupewa ofa ya kiungo wa kati wa Juventus na Brazil Arthur, 25, kama sehemu ya mkataba wowote kwa ajili ya klabu hiyo ya Italia ya kusaini mkataba na Digne. (Sport Mediaset - via Football Transfer Tavern)

Arsenal wanaangalia jinsi ya kuwahamisha wachezaji wawili kutoka Juventus - Winga Arthur na winga Mswiden Dejan Kulusevski, 21. (Marca)

Newcastle na West Ham wanafuatilia kwa karibu hali ya kiungo wa kati wa Tottenham Muingereza Dele Alli, 25. (Eurosport)

Newcastle wamempatia ofa kiungo wa mashambulizi wa kati wa Lyon Lucas Paqueta ya malipo ya pauni 181,457 kwa wiki ili ahamie katika kalbu hiyo ya St James' Park, ofa ambayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Brazili ameikataa kwasababu ofa hiyo haitakuwa sawa kimaslahi na ile anayopata kutoka Lyon. (Foot Mercato - in French)

Uhamisho wa beki wa Gremio Vanderson wa kuelekea Brentford unakaribia kukataliwa baada ya klabu hiyo ya Ligi ya 1 AS Monaco kuingilia kati na kutoa ofay a Euro milioni step 12 kwa Mrazili huyo mwenye umri wa miaka 20 . (Globo Esporte - in Portuguese) Wakala wa Erling Braut Haaland Mino Raiola amekanusha madai kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 wa Borussia Dortmund na Norway ana makubalianio ya awali ya kuhamia Real Madrid katika msimu ujao. (NOS - via Fabrizio Romano on Twitter)

West Ham wamefanya mawasiliano kwa ajili ya Rubin Kazan na mshambuliaji wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 21. (Football Insider)

Barcelona imekubaliana na masharti binafsi ya Ferran Torres lakini bado haijakamilisha mkataba kwa ajili ya mshambuliaji huyo Muhispania mwenye umri wa miaka 21 wa Manchester City. (Fabrizio Romano)

Juventus inataka kumhamisha mshambuliaji mwezi Januari huku Pierre-Emerick Aubameyang wa Arsenal , 32, Edinson Cavani wa Manchester United , 34, na Mauro Icardi wa Paris St-Germain , 28, wote wakiwa katika orodha ya wachezaji wanaowataka. (Tuttosport)

Aston Villa imetoa ofa kwa ajili ya mlinzi wa Liverpool na England Joe Gomez, 24. (CalcioMercato)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live