Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Disemba 20

Haqalandd Mshambuliaji wa Dortmund, Erling Braut Haaland

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi zinasema, Mkurugenzi mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke amethibitisha kwamba Real Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji Mnorway Erling Braut Haaland, 21.

Tetesi zinasema, Manchester City wako tayari kumuongeza mkataba kiungo, Bernardo Silva, 27 msimu huu, huku taarifa zikimuhusisha na kujiunga na Barcelona.

Mshambuliaji wa Fiorentina Mserbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 21, ambaye amekuwa akihusishwa na klabu za Manchester City, Arsenal na Newcastle, amekataa ofa ya hivi karibuni ya klabu yake .

Kiungo wa safu ya kati Mbrazili Fernandinho anaonekana yuko tayari kuendelea kubakia katika Manchester City mwezi Januari, huku matumaini ya kuhamia Atletico Mineiro kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36-yakififia.

Tetesi zinasema, Atletico Madrid watamuacha mlinzi wa England, Kieran Trippier, 31, ahamie katika Newcastle kwa pauni milioni 15, iwapo wanaweza kusaini mkataba na mchezaji mwingine mbadala.

Tetesi zinasema, Paris St-Germain wanataka kumsajili kiungo kinda wa Barcelona na Hispania Gavi, 17 katika dirisha dogo. Lakini mchezaji huyo anahitaji kusalia Nou Camp.

Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain Leonardo hakati tamaa kuhusu nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kusaini mkataba mpya licha ya kuhusishwa na Real Madrid.

Newcastle itaiacha Everton itatue suala la kuendelea kuwa na mlinzi wa Ufaransa asiye na furaha Lukas Digne, mwenye umri wa miaka 28.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live