Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka Barani Ulaya, Disemba 10

Foden Phil Foden

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: BBC Sports

Kiungo wa kati wa Manchester City na England Phil Foden, 21, ana thamani ya Pauni milioni 128 na ni miongoni mwa wachezaji ghali zaidi duniani. (Mail)

Real Madrid wana matumaini kwamba beki wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger , 28 ataweka mkataba wa awali na klabu hiyo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari na kujiunga nao katika uhamisho wa bila malipo msimu ujao. (The Athletic - subscription required)

Chelsea inalenga kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Real Madrid Casemiro, 29. (El Nacional - in Catalan)

Manchester City inataka kumpatia beki wa Ureno Joao Cancello , 27 kandarasi mpya. (Fabrizio Romano)

Ombi la West Ham la kutaka kumsajili mchaezaji wa Ulbegiji Eden Hazard kwa dau la Pauni milioni 21 limekataliwa na Real Madrid. (El Nacional - in Catalan)

Liverpool inawanyatia winga wa Leeds na Brazil Raphinha, 24, na mshambuliaji wa West Ham Jarrod Bowen, 24, kabla ya kuwasajili katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Liverpool Echo)

Liverpool pia inamchunguza mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 28. (Calciomercato - in Italian)

Mkufunzi wa Barcelona Xavi anatarajiwa kuamua kuhusu usajili wa mwezi Januari wa kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 24, Beki wa Marekani Sergino Dest, 21, na kipa wa Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 29.(Gerard Romero, via Sun)

Barca pia huenda ikamuuza kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 29, na beki wa Ufaransa Samuel Umtiti, 28. (Sport - in Spanish)

Borussia Dortmund wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Red Bull Salzburg na Ujerumani Karim Adeyemi,19, ambaye pia anahusishwa na klabu ya Bayern Munich na Liverpool. (Goal)

Paris St-Germain inataka kuwauza wachezaji mwezi januari , akiwemo mshambuliaji Mauro Icardi, 28, kiungo wa kati wa Brazil Rafinha, 28, na beki wa kati wa Senegal Abdou Diallo, 25. (L'Equipe - in French, subscription required)

Winga wa Real Madrid na Brazil winger Vinicius Junior, 21, amesema kwamba ana lengo la kutaka kusalia na klabu hiyo ya La Liga , akimuonya meneja wa klabu hiyo dhidi ya kutaka kumuuza. (Vamos, via Marca)

Chanzo: BBC Sports