Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi za Soka: Arsenal wamgeukia Cancelo

Joao Cancelo Arsenal Man City.png Tetesi za Soka: Arsenal wamgeukia Cancelo

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klab ya Arsenal italazimika kumsajili mlinzi wa kushoto Joao Concelo ikiwa wataamua kumuachia Kieren Tierney kwenda sehemu nyingine,

Pia kutokana na hali ya Majeruhi kwa Jurrien Timber Joao Concelo anatajwa kuwa ndiye mbadala wake ndani ya Arsenal.

Zipo taarifa zikimhusisha beki wa Arsenal Gabriel Magalheas [Mbrazili] kusajiliwa na moja ya klab ya Saudi Arabia.

Arsenal wanavutiwa sana kuipata huduma Laporte akitokea Manchester City, Lakini Manchester City kwa sasa hawana hamu tena ya kuwauzia Arsenal mchezaji wao.

Manchester United wanamtathimini kiungo wa Everton Amadou Onana, Lakini Sofyan Amrabat ndiyo kipaumbele nambari 1.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco amekuwa akiisubili Man United toka mwenzi June.

Bei ya pound million £70m plus £10m inaweza kuwa ya kutosha kwa West Ham United kumuuza kiungo wake Lucas Paqueta.

Manchester City wanarejea na ofa iliyoboreshwa kwa ajili ya kupata saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye tayari amekwisha fikia makubaliano binafsi na Man City.

Neymar anapanga kujiunga na Barcelona kama wakala huru mwaka 2025, jambo ambalo litamfanya kujiiandaa kwa kiwango kikubwa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2026.]

FC Barcelona wamefikia makubaliano kamili na João Cancelo juu ya masharti binafsi. Amekubali kupunguza mshahara mkubwa ili kusaidia klabu.

Sasa Barca lazima wakubaliane dili na Man City.

Klabu ya Al Hilal imefufu mpango wake wa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Fulham Aleksandar Mitrovic.

Bayern Munich wapo kwenye mazungumzo juu ya kumsajili Kipa wa Manchester City Stefan Ortega.

Newcastle United wanataka kumsajili beki mmoja wa kushoto kwa mkataba wa mkopo kati ya Kieran Tierney wa Arsenal au Marc Cucurella wa Chelsea.

Klabu ya Al Ahli wamekuba dili la kumsajili beki wa kati Merih Demiral kutoka Atalanta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live