Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi: Simba yamsajili Debora

Debora Fernandes Mavumbo Debora Fernandes Mavumbo

Thu, 27 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba inatajwa kukamilisha usajili wa kiungo kutoka Jamhuri ya Congo Debora Mavambo Fernandesn (pichani katikati) aliyekuwa aakiitumikia Mutondo Stars ya Ligi Kuu Zambia (MTN).

Kiungo huyo wa kati mzaliwa wa Angola mwenye umri wa miaka 24 tayari yuko nchini na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakaotambulishwa na Simba siku chache zijazo.

Debora ameitumikia Mutondo FC msimu mmoja akijiunga akitokea klabu ya Academica Petroleos do Lobito ya Angola mwaka 2023

Kiungo huyo anamudu kucheza eneo la kiungo mkabaji lakini pia mara chache ametumika katika safu ya ulinzi. Ujio wa Debora huenda ukashuhudia Simba ikiachana na Sadio Kanoute au Babacar Sarr.

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema uongozi uko kwenye majadiliano ya kusitisha mikataba ya baadhi ya wachezaji. Taarifa za wachezaji hao kupewa 'Thank You' zitatolewa baada ya michakato hiyo kumalizika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live