Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi: Dube anapasha misuli Avic Town

Dube Na Azam Kuanza Kupambana Kuanzia Kesho.jpeg Tetesi: Dube anapasha misuli Avic Town

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inaelezwa kuwa Mwana Mfalme Prince Mpumelelo Dube tayari ameshaanza mazoezi na Klabu ya Yanga kwa muda wa zaidi ya wiki sasa akiweka mwili wake sawa baada ya kuachana na Azam FC.

taarifa za ndani kutoka Yanga zinadai kuwa Prince Dube tayari ameshasaini mkataba wa awali na klabu ya Yanga kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao na mkataba huo ni wa miaka 2 kuichezea klabu ya Yanga baada ya kugomea ofa ya Simba.

Inaelezwa kuwa Dube alipoanza mazoezi siku ya kwanza alikabidhiwa jezi namba 9 iliyokua inavaliwa na Mshambuliaji kiongozi wa zamani wa klabu ya Yanga Fiston Mayele ila ameikataa na kuuomba uongozi umpatie jezi namba 29 aliyokua anavaa tangu yupo Azam Fc.

Klabu ya Yanga imemuaminisha Dube kuwa suala lilipo Kati yake na Klabu ya Azam litamalizwa muda si mrefu na yeye atakua huru. Clement Mzize atampisha Dube Young Africans.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live