Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi: Benchikha aomba kusepa Simba

Benchikha 0008 Kocha Benchikha

Sat, 27 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Abdelhak Benchikha ameupa taarifa uongozi wa Klabu ya Simba kuwa anahitaji kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, sababu ikiwa ni kuwa Simba haiwezi kufikia malengo yake anayohitaji kwenye michuano ya kimataifa.

Inaelezwa kuwa, Benchikha ambaye amehudumu Simba kwa takribani miezi 6, anahitaji kuondoka sababu nyingine ikiwa ni kuwa ana matatizo ya kifamilia kwao Algeria anahitaji kuondoka kushughulikia.

"Nimeomba kuondoka klabu mwishoni mwa msimu huu kutokana na sababu zangu binafsi (kifamilia) nahitaji kuwa nyumbani Algeria.

"Ligi ya hapa sidhani kama itaweza kunipa thamani pia nahitaji kubeba ubingwa wa Afrika kitu ambacho hakiwezekani kutokana na aina ya timu niliyonayo," amesema Kocha Abdelhak Benchikha.

Simba wao wamedai wanahitaji kuendelea nae kuelekea msimu ujao lakini Abdelhak Benchikha amesisitiza kuwa anahitaji kuondoka.

Niseme tu ukweli ikiwa akiondoka kabisa, basi Simba kuwa imepoteza kocha mzuri sana, angeweza kuwafikisha mahali fulani zaidi, lakini inaweza kuwa ni afya kwao kutafuta kocha mwingine mwenye falsafa za timu ya Simba (style of playing) lakini kwa Benchikha unapata nini?

1: Experience

2: Tactically

3: A great CV

Tena kwakuwa Simba wanastruggle kutinga nusu fainali klabu bingwa Afrika , nafikiri msimu ujao angewafikisha mahali pazuri na angeset vizuri timu kwa kuingia nayo pre season lakini maoni haya yanaweza kupotea kwa kiasi kikubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live